Kiwango cha Robin van Persie kimekuwa sio cha kuvutia msimu huu akifunga mabao 11 katika mechi 15 za ligi. Maneno yake kwamba wachezaji wenzao wanacheza kwenye maeneo ambayo yeye hupendelea kucheza yamezidi kuweka wasiwasi kwenye hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Pia
tetesi za kwamba mazoezi magumu ya Moyes hayamsaidii Van Persie zaidi
kumuongezea majeruhi - huku ikisemekana kwamba van Persie kwamba mbinu sahihi na
bora za mazoezi za kocha Rene Mulensteen ndizo zilizochangia kiwango kizuri
katika msimu wa kwanza wa Van Persie Old Trafford. Baada ya World Cup, mnamo
mwezi August Van Persie atakuwa na miaka 31, muda ambao mshambuliaji atakuwa
akitegemea zaidi namna ya kuji-position na umaliziaji kuliko
kasi.
Jukumu la RVP chini ya utawala David Moyes
Van Persie ni namba 9 na nusu, kama ambavyo anasemaga mwenyewe. Anapenda kurudi nyuma, kuanzisha mashambulizi na kwenda mbele kumalizia mashambulizi. Pia ni mzuri hewani na ndani ya box, ni mshambuliaji fundi na mmoja ya washambuliaji bora duniani. Dhidi ya Olympiakos, alipata nafasi moja nzuri ya kufunga baada ya kupokea krosi kutoka kwa Chris Smalling, lakini akauhamisha mpira upande wa kulia na kutoka nje ya mwamba, lakini unaweza kujiuliza kwanini United wanang'ang'ania kupiga makrosi kwa Rooney na Van Persie - washambuliaji hatari duniani wakati wanweza kumtumia kiungo mchezeshaji kuwapitishia mipira na wenyewe wamalizie.

Kwa macho tu,
ushirikiano wa Rooney na RVP unaonekana kuwa bora kabisa katika premier league,
hata barani ulaya. Lakini tatizo sasa ni kwamba Van Persie anacheza zaidi kama 9
kuliko navyocheza kama namba 10, ambapo inapaswa kwamba wakati RVP amerudi nyuma
Rooney aende mbele kucheza nafasi ya RVP, mabadilishano hayo sasa hayafanyiki
baina yao, aidha barani ulaya au kwenye premier league. Kama ambavyo katika
picha ya mchezo wa dhidi ya Olympiakos,. Rooney mara chache sana aliingia ndani
ya box, sababu kubwa haswa ni kutokucheza vizuri kwa mawinga pia huduma mbovu
kutoka kati kati ya kiwanja. Alichokuwa akifanya zaidi kuchukua mipira iliyokufa
kutoka Ashley Young na Antonio Valencia na kujaribu kumpelekea wachezaji wa
mbele.
Kuliko kucheza mfumo
wa 4-4-1-1 huku Rooney akiwa nyuma ya Van Persie, inaweza kuwa jambo la busara
kumchezesha Kagawa au Juan Mata nyuma ya RVP-Rooney katika mfumo wa Diamond au
4-3-1-2. Hili litapelekea wote wawili RVP na Rooney kuwavuta mabeki wa kati
pembeni, na hivyo kumuwezesha namba 10 aidha apige shuti kutokea nje ya box au
aingie ndani kupitia mwanya ulioachwa wazi na mabeki wa kati watakaokuwa
wakiwakaba RVP na Rooney.
Akiwa kwenye fomu
RVP ni mmoja ya washambuliaji bora barani ulaya lakini katika mfumo wa sasa wa
David Moyes anakuwa hapewi nafasi ya kutosha ya kurudi nyuma wala kucheza vizuri
na movements zake za kuwakimbia mabeki. Badala yake anaambiwa acheze ndani ya
box na jambo hilo linamlimiti kucheza katika ubora wake. Kwa mchezaji mkubwa
kama RVP, huu mfumo unamchosha na bila huduma bora kutoka kwa mawinga,
ataendelea kucheza chini ya kiwango.

HITIMISHO
Kwenye timu ya taifa Robin van Persie anae Arjen Robben ambaye hutokea upande wa kulia kuingia kati na kupenyeza mipira kati kati ya mabeki wa kati. Pia yupo Wesley Sneijder ambaye ni master pasi za mwisho kwa karibu na hata mipira mirefu. Anaweza pia kucheza nyuma ya namba 9 halisi kama Klaas-Jan Huntelaar, jukumu ambalo analiweza kisawa sawa, kutokana na ubunifu na ufundi alionao. Kwa Van Persie mchezo sasa wa United lazima acheze chini ya kiwango, United inabidi wabadilike kucheza bila mawinga halisi, Mata na Kagawa wanaweza kuchukua mashavu wakicheza kama viungo washambuliaji wanaoingia ndani - wakimtegemea Rooney kupandisha timu mbele na pia kuongeza wa wachezaji wa United katikati - eneo ambalo United wamekuwa dhaifu kwa misimu kadhaa sasa.
src
Shaffihdauda

0 comments:
Post a Comment