Dodoma. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge na kusema uvumilivu una kikomo chake.

Aliyasema hayo jana wakati anafungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, kilicholenga kuweka msimamo wa chama kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya ambayo inaanza kujadiliwa Jumanne wiki ijayo.
“Tuna uchaguzi mdogo, Iringa, Kalenga, tumeshapata mgombea na tumefanya hiyo kazi kwa niaba yenu kwa sababu hatukupata muda wa kuitisha Kikao cha Halmashauri Kuu, lakini mmetupatia mamlaka ya kufanya hivyo na Katiba imetupa fursa ya kufanya uteuzi kwa niaba yenu,”alisema.
CCM imemteua Godfrey Mgimwa ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Dk William Mgimwa, kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye mwaka huu. Dk Mgimwa hadi anafariki dunia alikuwa Waziri wa Fedha.

Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge na kusema uvumilivu una kikomo chake.
Aliyasema hayo jana wakati anafungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, kilicholenga kuweka msimamo wa chama kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya ambayo inaanza kujadiliwa Jumanne wiki ijayo.

“Tuna uchaguzi mdogo, Iringa, Kalenga, tumeshapata mgombea na tumefanya hiyo kazi kwa niaba yenu kwa sababu hatukupata muda wa kuitisha Kikao cha Halmashauri Kuu, lakini mmetupatia mamlaka ya kufanya hivyo na Katiba imetupa fursa ya kufanya uteuzi kwa niaba yenu,”alisema.
CCM imemteua Godfrey Mgimwa ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Dk William Mgimwa, kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye mwaka huu. Dk Mgimwa hadi anafariki dunia alikuwa Waziri wa Fedha.

Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani
“Mpaka sasa kwa dalili tulizonazo hatuna mgawanyiko wala hakuna misukosuko maana lile la Arumeru (uchaguzi mdogo katika Jimbo la Arumeru Mashariki) lilikuwa na misukosuko tangu tumeanza hadi tumemaliza,” alisema.

Katika uchaguzi huo, uliofanyika Aprili mosi, 2012 mgombea wa Chadema, Joshua Nassari aliibuka mshindi baada ya kumshinda Sioi Sumari wa CCM ambaye ni mtoto wa marehemu Jeremiah Sumari, aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi mwaka 2008 hadi 2010.
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi na wanachama wa CCM katika kata 23, ambazo CCM iliibuka na ushindi na kuwataka kuweka nguvu zaidi katika kuzikomboa kata nne zilizoangukia mikononi mwa wapinzani.

Kata ambazo wapinzani walishinda ni Sombetini (Arusha Mjini), Kiboroloni (Moshi Mjini), (Njombe Mjini),zote zilichukuliwa na Chadema. Kilelema mkoani Kigoma (NCCR Mageuzi).
Aidha, Rais Kikwete alisema awali wakati wanaahirisha kikao cha Nec kilichopita, walikubaliana watakuwa wakihamia mikoani kufanya vikao hivyo ambapo Mbeya waliomba kuwa wenyeji na walikubaliwa.

Hata hivyo, alisema waliamua kufanya tena kikao hicho mjini hapa, kwa sababu ya agenda watakazozizungumza kwenye kikao hicho ambazo ni suala linalohusu mchakato wa Katiba Mpya.
“Ili tutakapoyamaliza, tujue tuweke misimamo gani itakayokwenda kwenye Bunge la Katiba. Haina maana kuwa ile agenda yetu ya Mbeya tumeifuta, ahadi iko palepale, kikao kitakachofuata cha kawaida kitafanyikia Mbeya,”alisema.

Awali Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimkaribisha Rais Kikwete, alisema kuwa wajumbe wa Nec ni 372, lakini waliohudhuria walikuwa ni 368 (sawa na asilimia 98.3) hadi kikao kinafunguliwa.
source
mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Top