Uraia haubinafsishwi na mwekezaji wa kweli haulizwi uraia
Toleo la 340
26 Feb 2014
BILA shaka wengi tunakumbuka kwa uchungu kabisa jinsi tulivyoshuhudia
viwanda vilivyotengenezwa kwa mikopo ambayo ni sehemu ya deni la
Taifa, vilivyouzwa kwa bei ya ’kutupa’ kwa wanaoitwa ’wawekezaji’.
Wengi wa ’wawekezaji’ hawa walichofanya ni kugeuza viwanda vile kuwa maghala na kuuza majumba na mtandao wa rasilimali ambazo zilikuwa chini ya viwanda; na kwa kuwa hawakuwa na nia hasa ya kuzalisha wengi waliuza mitambo au waliitelekeza kwa walinzi ambao hawakuwa na mwajiri wa moja kwa moja, kufanya walinzi wale waendelee kujilipa ’mishahara’ kwa kuuza mitambo ile ya gharama katika vipande vidogo vidogo kama vyuma chakavu.
Matokeo ya ubinafshaji katika maisha ya wanachi yalishuhudiwa kwa katika eneo la ukosefu wa ajira, ajira isiyo na uhakika na kutokuwa na hakika ya maisha ya kila siku na kupanda kwa gharama zisizoepukika za maisha.
Hiki ndicho kipindi ambacho nchi yetu ilishuhudia kina ’Ngapulila’ wengi ambao kwenda nje kutafuta maisha ndio lilikuwa suluhisho pekee la matatizo yao ya kiuchumi waliyokuwa wakipambana nayo, ambayo kwa bahati mbaya na kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yao walijikuta hawakuwa na mtu wa kuwasemea.
Ikumbukwe, msingi mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Azimio la Arusha ilikuwa ni kuwasemea wanyonge, ’kubatilishwa’ kwa Azimio la Arusha kule Zanzibar na kuachia nguvu ya ’mitaji’ kutamalaki, kulidhoofisha sana misingi ya utu na imani ya watu kwa serikali yao.
Walioondoka wakati ule wengi wao walikuwa ’waathirika’ wa mabadiliko yale yaliyoruhusu ubinafsishaji katika sekta zote muhimu, na ndiyo hawa tunawazungumzia leo kama ’diaspora’.
Kati ya masuala yanayozungumzwa sana ni kuruhusu uraia-pacha. Naamini na nimepata kusikia mara kwa mara viongozi wetu waandamizi wakitoa kauli za kukubaliana na suala hili la kuruhusu uraia-pacha wakitumia sababu zile zile walizotumia kwenye ubinafsishaji wa viwanda; sababu kuu inayotumika sasa katika kutaka kuhalalisha ’uraia-pacha’ eti ni kuvutia mitaji, kuongeza ajira na kuongeza pato la serikali kupitia kodi.
Imekuwa ni mazoea kwetu kuenenda kwa matukio. Kufanya maamuzi makubwa na yenye athari kubwa kwa spidi ya ’kufa mtu’. Kwa sababu hii, mara kwa mara tumejikuta tukifanya makosa, na kwa kuwa tu wazito kutambua makosa yetu, mara kwa mara tumejikuta tukirudia makosa yale yale, kwa kuwa hatujifunzi.
Safari hii pia, suala la uraia-pacha ’tumeshauriwa’ na sasa utekelezaji wake ni moja ya mambo yanayoenda kwa kasi kubwa, kwa hulka yetu si jambo la kustaajabisha. La kustaajabisha hapa ni jinsi gani suala hili linavyopelekwa-pelekwa, ni suala linalostaajabisha kwa kila mtu anayetaka kujisumbua kujifikirisha.
Kwa kuwa nchi yetu imejaa ’wawekezaji’ kutoka kila taifa, bila shaka wengi wangetamani kuitumia fursa hii; swali ni kwa kiasi gani uraia huu pacha utaendelea kuwafaidisha wengine (Wazungu, Wachina na wahamiaji wengine) na si Watanzania ni swali linalohitaji mjadala, lakini dalili za mvua ni mawingu.
Kuna kila dalili, suala hili linashabihiana kama ilivyo kwa wawekezaji wakati tunawafungulia milango, Watanzania waliaminishwa ’uwekezaji’ ni kwa faida ya Watanzania, kwa kuwa umasikini wetu umetokana na kutokuwa na mitaji. Kilichotokea kila mtu anafahamu, Watanzania waligeuka manamba kwenye nchi yao, na kwa kuwa tumecheza na hatima yetu katika maeneo nyeti tumebaki watazamaji pale raia wa nje wanapokuja kuchukua fursa za kazi, biashara na uwekezaji.
Kama ilivyo katika uwekezaji, uraia wa nchi pacha hauna hakika kama utamnufaisha Mtanzania aliyepo Tanzania au yule aliye ughaibuni. Hata kama wenzetu wamefaidika nao, mazingira ya Tanzania ni tofauti na wenzetu, na hata sababu za Watanzania kuondoka na kuishia ughaibuni hazishabihiani kihivyo na wengine.
Hivyo basi utafiti ni muhimu kufanyanyika kabla ya maamuzi. Bila utafiti haiyumkini uamuzi huu ukawa na athari za muda mrefu; hata kama utawafaidisha Watanzania wasiozidi milioni tatu wanaoishi nje, ukawa janga kwa Watanzania zaidi ya milioni 42 wanaoishi Tanzania, na kwa hakika fursa chache zilizopo na zilizotengwa kwa ajili ya Watanzania zikapotea hasa kwa kuwa kuna kila dalili kuwa ’wawekezaji’ walio nyumbani ndio watakaochangamkia zaidi ’fursa’ hii.
Haishangazi basi, suala hili la uraia pacha linachagizwa na serikali za nje kama Canada na Oman (ndizo zilizotajwa) na kuingizwa kwenye ajenda kama mahitaji muhimu ya Watanzania wanaoishi nje. Swali la kujiuliza hapa kwa nini Canada na Oman ndizo vipaumbele na si Afrika Kusini, au Ulaya?
Sipendi kuhisi, lakini isije ikawa huu ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu kuwarudisha wale waliokimbia Azimio la Arusha na Mapinduzi ya Zanzibar kwa mlango wa nyuma, hasa kwa kuwa mpango huu unawezeshwa na serikali hizo (rejea Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje Uk. 43-44)
Kama ilivyo muhimu kuwa na sera ya madini kabla kuuzwa kwa vitalu, vivyo hivyo kuna umuhimu wa kuwa na sera ya ”Watanzania wanaoishi nje” kabla hatujaruhusu kinachoitwa ”uraia-pacha”. Ni muhimu sana kuwa na sera ambayo Watanzania wanaoishi nje na wadau wa nyumbani wakashiriki kuitengeneza. Mchakato wa kuitengeneza sera hii haiyumkini utatoa nafasi kwa serikali kuwafahamu hao ”diaspora” ni kina nani, wanafanya nini, wako wapi, na maeneo gani ya kimkakati tunahitaji kushirikiana nao katika kuiendeleza nchi yetu.
Matokeo ya kitaalamu na kitafiti yanaweza kutoa mwelekeo mzuri katika kuangalia njia bora zaidi ambayo serikali inaweza kuitumia kuwaleta karibu Watanzania (pengine bila hata ya kulazimika kuwa na uraia-pacha).
Ifahamike kuwa ni nchi chache sana ambazo zinatoa uraia-pacha usio na masharti tena kwa sababu za kimkakati. Nchi nyingi zinatumia njia mbalimbali na tofauti kuwafanya wananchi kuwa sehemu ya nchi wanazotoka na kuwafanya wawajibike katika kushiri katika juhudi za maendeleo.
Mexico wana mpango unaitwa ’Tres Por Uno (3x1)’ ambao unamuwezesha kila diaspora anayetuma pesa moja nyumbani kuwekeza, serikali inamuongea 3; mpango huu ni bora na nafuu zaidi kuvutia uwekezaji kuliko ule wa kusamehe kodi ’wawekezaji’; njia nyingine ya kuvutia diaspora ni pamoja na kutambuliwa na kuchukuliwa kama raia ikiwemo kupewa hadhi maalumu ya ukazi ambao hauna masharti kwa mwananchi yeyote anayeamua kurudi kufanya kazi au kuwekeza (Ethiopia wana utarativu wa yellow card)
Pamoja na hayo, serikali inaweza kutathmini changamoto wanazokumbana nazo Watanzania nje na kuangalia ni jinsi gani na kwa kiasi gani serikali inaweza kubeba baadhi ya changamoto ambazo zipo nje ya uwezo wa diaspora wenyewe, kurahisisha maisha yao na kushiriki kwa karibu katika ujenzi wa Taifa, changamoto hizi ni kama gharama ya usafirishaji pesa nyumbani (ambazo ni kubwa ukilinganisha na nchi nyingine za jumuiya ya Afrika Mashariki), haki za Watanzania wanaoishi nje, na hata kubadilishana kodi na nchi nyingine (kama nchi zinavyobadilishana wafungwa).
Ingawa tumebinafsisha vingi, bado hatujachelewa, kuna vingine hatupaswi kuvibinafsisha, uraia ni suala mojawapo

Mheshimiwa Spika,Kama ilivyo gesi na madini, suala la sera lilikuwa ni muhimu sana katika mjadala na kwa kiasi kikubwa watu walijiuliza; ”hii kasi yote ni ya nini?”
...katika mwaka huuwa fedha, Wizara yangu imechukua jitihada zamakusudi za kupanua wigo kwa kuwafikia Diaspora waishio Canada na Oman. Mikutano na Watanzania hao iliandaliwa sanjari na ziara za Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika nchi hizo mwezi Oktoba 2012. Nchi hizi mbili, kwanza zina Watanzania wengi walio jizatiti kiuchumi, kijamii na hata kisiasa. Lakini pili, Serikali za nchi hizo zinaunga mkono jitahada zetu na zipo tayari si tu kuwawezesha ila kushirikiana na Diaspora hao kuchangia maendeleo ya nchi yetu.
Kama ilivyo muhimu kuwa na sera ya madini kabla kuuzwa kwa vitalu, vivyo hivyo kuna umuhimu wa kuwa na sera ya ”Watanzania wanaoishi nje” kabla hatujaruhusu kinachoitwa ”uraia-pacha”. Ni muhimu sana kuwa na sera ambayo Watanzania wanaoishi nje na wadau wa nyumbani wakashiriki kuitengeneza. Mchakato wa kuitengeneza sera hii haiyumkini utatoa nafasi kwa serikali kuwafahamu hao ”diaspora” ni kina nani, wanafanya nini, wako wapi, na maeneo gani ya kimkakati tunahitaji kushirikiana nao katika kuiendeleza nchi yetu.
Matokeo ya kitaalamu na kitafiti yanaweza kutoa mwelekeo mzuri katika kuangalia njia bora zaidi ambayo serikali inaweza kuitumia kuwaleta karibu Watanzania (pengine bila hata ya kulazimika kuwa na uraia-pacha).
Ifahamike kuwa ni nchi chache sana ambazo zinatoa uraia-pacha usio na masharti tena kwa sababu za kimkakati. Nchi nyingi zinatumia njia mbalimbali na tofauti kuwafanya wananchi kuwa sehemu ya nchi wanazotoka na kuwafanya wawajibike katika kushiri katika juhudi za maendeleo.
Mexico wana mpango unaitwa ’Tres Por Uno (3x1)’ ambao unamuwezesha kila diaspora anayetuma pesa moja nyumbani kuwekeza, serikali inamuongea 3; mpango huu ni bora na nafuu zaidi kuvutia uwekezaji kuliko ule wa kusamehe kodi ’wawekezaji’; njia nyingine ya kuvutia diaspora ni pamoja na kutambuliwa na kuchukuliwa kama raia ikiwemo kupewa hadhi maalumu ya ukazi ambao hauna masharti kwa mwananchi yeyote anayeamua kurudi kufanya kazi au kuwekeza (Ethiopia wana utarativu wa yellow card)
Pamoja na hayo, serikali inaweza kutathmini changamoto wanazokumbana nazo Watanzania nje na kuangalia ni jinsi gani na kwa kiasi gani serikali inaweza kubeba baadhi ya changamoto ambazo zipo nje ya uwezo wa diaspora wenyewe, kurahisisha maisha yao na kushiriki kwa karibu katika ujenzi wa Taifa, changamoto hizi ni kama gharama ya usafirishaji pesa nyumbani (ambazo ni kubwa ukilinganisha na nchi nyingine za jumuiya ya Afrika Mashariki), haki za Watanzania wanaoishi nje, na hata kubadilishana kodi na nchi nyingine (kama nchi zinavyobadilishana wafungwa).
Ingawa tumebinafsisha vingi, bado hatujachelewa, kuna vingine hatupaswi kuvibinafsisha, uraia ni suala mojawapo
0 comments:
Post a Comment