Bagamoyo. Vyama vinne vimejitokeza kusimamisha wagombea wao ili wapambane na Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwan Kikwete ambaye tayari amepitishwa na chama hicho tawala kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Ofisa Uchaguzi wa Wilaya ya Bagamoyo, David Shija alivitaja vyama hivyo kuwa ni pamoja na Chadema ambacho kimemsimamisha Mathayo Torongei, Chama cha Wananchi (CUF) kilichomteua Fabian Skauki, NRA kimemsimamisha Muniru Hussein na AFP ni Ramadhani Mgaya.
Alisema mchakato wa kuchukua fomu na kurudisha utafungwa Machi 12 alasiri, saa 10 na kwamba uteuzi wa wagombea utafanyika siku hiyo na Machi 13, kampeni kwa kila chama zitaanza rasmi.
“Vyama vitano vya siasa ndivyo hadi sasa vilivyofika ofisini ambapo walichukua fomu za kushiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze,” alisema Shija msimamizi wa uchaguzi.
src
mwananchi
Katika hatua nyingine, mgombea ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama cha AFP, Ramadhani Mgaya alisema chama chao katika kampeni zinazotarajia kuanza hivi karibuni kimejipanga kutumia rasilimaliwatu na si rasilimalifedha. Mgaya alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu juzi jioni kwenye ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilayani humo.
“Vipo baadhi ya vyama nchini ni matajiri na wanawasimamisha matajiri kwa sababu wana jeuri ya kutumia fedha kurubuni wananchi,”alisema Mgaya.
Mgombea huyo wa AFP alisema gharama za uchaguzi katika jimbo zinatakiwa zisizidi Sh50 milioni lakini gharama hiyo imekuwa ikizidishwa na baadhi ya vyama vyenye majina, hivyo kuvunja sheria ya uchaguzi iliyowekwa.
Uchaguzi wa kuwania ubunge katika Jimbo la Chalinze utafanyika Aprili 6, mwaka huu ikiwa ni kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Said Bwanamdogo aliyefariki dunia mapema mwaka huu.
src
mwananchi
0 comments:
Post a Comment