Na
Baraka Mpenja, Dar Es Salaam
0712461976
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea
kesho katika raundi ya 25 ambapoTanzania
Prisons na Rhino Rangers wataumana Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini
Mbeya) wakati Coastal Union watakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi
hiyo itaendelea Keshokutwa (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi nyingine tano za
kukamilisha raundi hiyo.
Simba watavaana na Ashanti United Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Uwanja
wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Mtibwa
Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting
na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku
Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya.
Kesho
mtandao huu utakupatia uchambuzi mwingine kuelekea mechi hizo za keshokutwa ili
kubashiri ni timu gani inaweza kushinda.
SIMBA
VS ASHANT UNITED
Hii
ni mechi yenye mvuto kwa kuangalia umuhimu wa matokeo kwa Ashanti United waliopo
katika hatari kubwa ya kushuka daraja.
Ashanti
wamecheza mechi 24 na kufanikiwa kushinda mechi 5, sare 7 na kupoteza mechi 12,
hivyo kujikusanyia pointi 22 katika nafasi ya 12.
Mbele
ya Ashanti United wapo Tanzania Prisons waliocheza mechi 24 ambapo wameshinda
mechi 4, sare 10 na kufungwa mechi 10.
Kinachowafanya
Prisons wawe juu ya Ashanti ni wastani mzuri wa mabao ya kufunga na
kufungwa.
Prisons
wamefunga mabao 21 na kufungwa mabao 30. Ukitoa mabao ya kufunga na kufunga
unapata hasi tisa (-9).
Ashanti
wamefunga mabao 19 na kufungwa mabao 38, hivyo ukitoa mabao ya kufunga na
kufungwa unapata hasi kumi na tisa (-19).
Kwa
hesabu hizo, Prisons wanakuwa juu ya Ashanti hata kama wote wana pointi 22
katika michezo yao 24 waliyoshuka dimbani.
Kwa
mazingira haya ya Ashanti United, mechi ya keshokutwa ni muhimu sana, tena
wanahitaji kushinda mabao mengi zaidi kwasababu hata Prisons watakuwa na mchezo
dhidi ya vibonde Rhino Rangers kutoka mjini Tabora katika uwanja wao wa Sokoine
jiji Mbeya.
Simba
sc hawana cha kupoteza mpaka sasa, hawawezi kutwaa ubingwa wala kushika nafasi
tatu za juu kwa pointi zao 37, huku wakibakiza mechi mbili
tu.
Endapo
Simba sc watashinda mechi zote watafikisha pointi 43 ambazo zilishavukwa na
Mbeya City walioopo nafasi ya tatu.
Hivyo
Simba baishara yao ni nafasi ya nne ambayo wanapambana na Kagera Sugar wenye
pointi 34 katika nafasi ya tano, huku wakibakiza mechi
mbili.
Kama
Kagera Sugar watashinda mechi zote watafikisha pointi 40, na ili kuipata nafasi
ya nne watatakiwa kuwaombea Simba wapoteze mechi zote mbili.
Simba
sc kwasasa wanahitaji heshima tu kwa kushinda mechi zao
zilizobaki.
Kwa
mazingira hayo bila shaka wamejiandaa vizuri kuwafunga Ashanti United keshokutwa
katika dimba la Taifa.
Kocha
Mkuu wa Simba sc, Mcroatia Dravko Logarusic ataingia uwanjani kwa kusaka ushindi
mbele ya kocha wa Ashanti Abadallal Kibadeni “King Mputa”.
Huu
utakuwa mchezo mgumu zaidi kwa Kibadeni kwasababu matokeo yanayomfaa kwakwe ni
ushindi tu.
Kama
atashinda mechi ya keshokutwa itakuwa faida kubwa kwake. Kwa mana hiyo kesho
ataingia kwa nia ya kushambulia na kulinda lango lake kwa muda
wote.
Simba
na Ashanti wana malengo tafauti kabisa kwasababu Simba wanahitaji kulinda
heshima, wakati Ashanti wanataka kukwepa kushuka daraja.
Mtumwa
zaidi katika mechi hiyo ni Ashanti kwasababu pointi tatu zitaamua hatima yao,
wakati Simba kwao hata kama wakizikosa hakuna madhara ya kushuka
daraja.
Hii
itakuwa mechi nzuri ya kuifuatilia kwani soka la ushindani na maarifa linaweza
kuonekana hasa kutoka kwa Kibadeni ambaye mzunguko wa kwanza alikuwa kocha mkuu
wa Simba.
Kwa
kiasi fulani Kibadeni anawafahamu wachezaji wa Simba na utamaduni wao, hivyo
inaweza kuwa faida kwake.
Inadhihirika
wazi kuwa kucheza na timu inayokwepa kushuka daraja, mechi inakuwa ngumu zaidi,
kwasababu hiyo, Loga wa Simba sc lazima awe na mipango mizuri na asipoangalia
anaweza kupoteza mechi hiyo.
TANZANIA
PRISONS VS RHINO RANGERS
Wakati
Ashanti wakiumiza kichwa kupata matokeo katika mechi hiyonya jumapili, nao
Tanzania Prisons ambao ni washindani wao kukwepa kushuka daraja watakuwa na
vibonde wa ligi hiyo, Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora katika uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya siku ya kesho.
Pengine
mechi hii itakuwa na unafuu kwa Prisons wanye machungu ya kufungwa mechi mbili
zilizopita.
Walifungwa
mabao 5-0 dhidi ya Yanga na wakafungwa mabao 21 na JKT Oljoro mjini Arusha. Sasa
kesho wapo nyumbani kucheza na timu dhaifu ya Rhino Rangers.
Udhaifu
unaosemwa hapa ni matokeo wayapatayo Rhino msimu huu, lakini si jinsi
wanavyocheza.
Wanajeshi
hawa JWTZ wanacheza mpira mzuri, lakini katika mpira mshindi na mshindwa lazima
atokee.
Kwa
maana hiyo, Prisons wana kazi kubwa ya kuwafunga vibonde hawa walipo mkiani kwa
pointi 16 baada ya kucheza mechi 24.
Mechi
hii haina mvuto hata kwa mashabiki wa soka jijini Mbeya kutokana na matokeo
waliyonayo Prisons na Rhino, lakini kwa watu wa mpira, hii ni mechi ambayo
burudani kubwa inaweza kuonekana.
Prisons
watashinikiza kushinda, wakati Rhino ambao wameshashuka daraja kwa asilimia zote
watakuwa wanapambana angalau kushuka daraja na ushindi.
COASTAL
UNION VS JKT RUVU
Mechi
nyingine nzuri ya kesho ni baina ya Coastal Union dhidi ya JKT Ruvu katika
uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Coastal
walipoteza mechi iliyopita kwa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo katika uwanja wa
Mkwakwani, wakati JKT Ruvu walipoteza kwa mabao 5-1 kutoka kwa mabingwa watetezi
Yanga ndani ya uwanja wa Taifa.
Mtazamo
wa mechi hii kwa timu zote mbili unatofautina kabisa.
JKT
Ruvu wenye pointi 28 katika nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 24 watakuwa
wanahitaji ushindi ili kufikisha pointi 31 ambazo zitaweza kuwaokoa kushuka
daraja.
Hata
sare itakuwa na faida kubwa zaidi kwao, kwasababu watafikisha pointi 29 ambazo
hazitaweza kufikiwa na Ashanti United na Prisons isipokuwa Mgambo waliopo nafasi
ya 10 kwa pointi 25 huku wakiwa na michezo miwili mkononi.
Coastal
Union wapo nafasi ya 8 kwa pointi 29 baada ya kucheza mechi 24. Nafasi hii si
nzuri kwao kwasababu ya kikosi chao kuwa na wachezaji wa
gharama.
Kikosi
cha wagosi wa Kaya kilitabiriwa kufanya vizuri sana msimu huu, lakini wamegeuka
kuwa `mbogo` kwani wanapoteza mechi mara kwa mara.
Kwahiyo
mechi ya Mkwakwani itakuwa nzuri kwasababu timu zote zinahitaji ushindi ili
kuendelea kujiweka mazingira mazuri zaidi katika msimamo.
Tafadhali
endelea kuwa nasi na usisite kutoa maoni yako.
src
shaffih dauda
0 comments:
Post a Comment