Ama kweli kila nyuma ya mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke imara.Hili limejidhihirisha mwishoni mwa wiki iliyopita wakati msanii kiwango wa bongo fleva Naseeb Abdul 'Diamond Plutnumz' alipoweka rekodi ya msanii aliyechukua tuzo nyingi za Kili Music tangu tuzo hizo zianzishwe.....
Diamond akiwa ameongozana na mpenzi wake Wema Sepetu kwenye tuzo hizo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar alionekana kuwa na furaha muda wote wakati wa kwenda kuchukua tuzo hizo....
Diamond alizoa tuzo 7 na kuacha gumzo ikiwa ni mafanikio yake makubwa kuwahi kuyatapata tangu tuzo hizo zianzishwe akiivunja na kuipita rekodi ya 20% aliyewahi kuchukua tuzo 5 mwaka 2011....
Akiongozana na mpenzi wake katika kila tuzo, Diamond alikiri kuwa tuzo hizo ni kwa ajili ya baby wake huyo ( Wema ) huku akimshukuru pia mama yake na kampani yake....
Ni muda sasa uhusiano kati ya Wema na Diamond umekuwa ukigonga vichwa vya habari katika sura tofautitofauti huku wawili hao wakiendelea kupambana na hali hiyo....
Wema ameonekana kujirekebisha kwa wakati huu ambao amerudiana na Diamond tofauti na walivyokuwa awali....
Uhusiano wao umeteka hisia za watanzania wengi kutokana na matukio mengi yanayowaandama ikiwemo mama Wema kuingilia mapenzi yao na pia mama Diamond kutopendezwa na uhusiano huo huku akipendekeza Penniel Mungilwa 'Penny' kuwa mpenzi wa mwanae....
Watu wa karibu na Diamond wanaopingana na mama Diamond huku wakimpendekeza Wema wamedai kuwa Wema Sepetu ana kismati na Diamond tofauti na ilivyo kwa Penny....
Wakiendelea kufunguka, watu hao waliweka wazi kuwa wakati wote Diamond anapokuwa na Wema hung'aa tofauti na alivyokuwa na Penny ambapo kila kitu kilirudi nyuma....
"Nakwambia Diamond asingecheza karata dume ya kurudiana na Wema,sasa hivi angekuwa katika hali mbaya sana,sema nina msifu anaakili za kuzaliwa na anajua kusoma alama za nyakati" Alisema ndugu mmoja aliyekataa kuandikwa jina lake
Akifunguka hivi karibuni, mtangazaji mmoja wa redio maarufu hapa nchini ameeleza kuwa hata tuzo alizopata Diamond, Wema anahusika kwa kuwa anamvuto wa ajabu....
"Diamond sasa hivi hana haja tena ya kwenda kwa waganga, maana kuna tetesi hizo.Wema ni kama hirizi yake,yaani kila anapogusa ni balaa.Huyo Penny kama alikuwa anasubiria kuolewa atasubiria miaka mia" alimalizia mtangazaji huyo
src
eddy blog
0 comments:
Post a Comment