Niaje…niaje wanangu hapo kwa fasi ya kitaa? Ama nini? Kama mpo biyee basi mzuka machalii wangu.
Tudei bana ngoja tugonge stori za kitaani kwangu. Aisee pale kitaani kuna drama hatari. Weka mbali na majanki!
Ni hapa tu kwa fasi ya Sinza, Bongo tambarare wanangu kama vipi mnaweza kujisogeza kitaa hiki tuone inakuwa nini!Mzazi nikisema nikupe ishu moko afta nyingine ni parefu hata gazeti lote halitoshi bati ngoja nikumegee hapo hii moko dheni mambo mengine tutajua fowadi.
Labda tofauti na kitaa kingine bati kwenye kitaa ninachochili pipo tunanyakana mwanzo mwisho.
Yule fulani anatoka na fulani, sasa basi kuna jamaa yetu bwana alikuwa anaminya na waifu wa msela kwa muda mrefu kinoma na pipo kitaani wananyaka mchongo mzima.
Mwana  ana eji kama ya miaka dheti na shori ana eji hiyohiyo so wanasomana na jamaa.
Basi bwana mshikaji akawa anajisevia kama kaoa vile, mahaba nikaangarize yakanoga. Unajua malovee yakinoga ile mbaya huwa wana wanajisahau au kujitoa fahamu.
Mwanangu akawa anapelekewa menyu geto nini na nini hadi mchizi akaona laifu linataka nini sasa.
Laifu likaendelea kunoga zaidi na zaidi, mchizi alikuwa ana mtoto alizaa na demu mwingine akawa anampeleka kushinda na yule shori wa mtu dei nzima.
Wakati yanafanyika hayo yote mume wa yule mtoto mkare alikuwa anaona na anajua mpango mzima ila aliuchuna kama hajui lolote ila ukweli ni kwamba alikuwa ananyaka kila kitu.Kama mjuavyo washikaji samutaimu tukichili mageto huwa tunapiga stori zinazowahusu watoto wazuri.
Kuna dei bwana niliimuuliza mchizi kuhusu uhusiano wake na yule shori mke wa mtu kwamba hazibendi wake anachukuliaje ukizingatia jamaa anajua kila kitu.Msela alichojibu ni kwamba jamaa haongei kitu kwa mkewe kwa rizoni kwamba waifu wake kamtengeneza kinoma so hapindui.
Basi bana, yule waifu wa msela akabeba pregi na ikawa bigi kama miezi sita hivi. Huku na huku kukatokea mzinguo kati ya msela na huyo waifu wa mwana.Unaambiwa yule shori akaamua kuitoa ile mimba. Kitendo cha kuitoa mchizi akamaindi ileile, akamwita shori kwa geto kwake akampa vitasa vya kutosha nusu amtoe kitu cha pumzi kama siyo majirani kuvunja mlango.
Unaambiwa shori alipotimba maskani mumewe akamuona na manundu, kuuliza vipi mai waifu akawa anajiumauma, msela akajua aliyefanya mambo ni mchizi.Alichokifanya hazibendi ni kumfuata kachala kwa fasi ya geto na kumteli kwamba alipofikia sipo so akamteli kuwa yeye siyo mburura kama waifu wake amemtengeneza.
Akaona isiwe kitu, amfungukie tu kwamba yeye na mai waifu wake ni waathirika wa ngoma yaani Ukimwi tangu kitambo.Akamsanua kwamba kutembea na mke wake siyo mbaya ila ishu za kumpiga siyo kabisa dheni baada ya kumwambia hivyo akajikata.
Alichokifanya mwana ni kwenda kupima dheni akakuta kweli ana ngoma so yupo kwenye matumizi ya vidonge. Kuna ishu ukizipiga masti ujifikirie maana emsii wa msiba huwa hapigiwi makofi.Mmenisoma? Acha kushoboka wewe! Angalia mbele. Sii yuu neksti wiki!

0 comments:

Post a Comment

 
Top