John Kerry asema Uganda inakiuka haki za
binaadamu
Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria
dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema tangu Uganda
iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita, Marekani ilieleza wazi kwamba
sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha kuwepo haki za binaadamu ambalo tume
ya haki za binaadamu Uganda inatambua linaambatana na sheria ya Uganda
Sheria mpya imezusha hisia kali
Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.
Marekani inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake na kutishia jamii ya wapenzi wa jinsia moja Uganda
SRC
BBC
0 comments:
Post a Comment