Dodoma. Kiasi cha Sh8.2 bilioni
kimetumika kufanya ukarabati mkubwa wa Ukumbi wa Bunge pamoja na miundombinu
yake kwa ajili ya shughuli za Bunge la Katiba litakalokutana kwa zaidi ya siku
70. Mbali ya gharama hizo, imeelezwa pia kuwa kila mbunge wa Bunge hilo maalumu
la Katiba atalipwa Sh300,000 kwa siku katika kipindi chote litakapokuwa
linakutana.
Katibu
wa Bunge, Dk Thomas Kashililah aliwaambia waandishi habari Mjini Dodoma jana
kuwa posho hizo za wabunge zimechanganuliwa katika sehemu mbili.
Alisema
Sh220,000 ni kwa ajili ya posho ya kikao, usafiri na dereva na Sh80,000 ni
posho ya kujikimu na kwamba hicho ndicho kiwango kilichoidhinishwa na Rais
Jakaya Kikwete.
“Tuliposikia
kuwa wabunge watalipwa posho ya Sh700,000 kwa siku na sisi hatukujua ilitokea
wapi kwa sababu Rais hakuidhinisha malipo ya aina hiyo,” alisema Dk Kashililah.
Gharama za ukarabati
Kuhusu
ukarabati wa ukumbi na miundombinu yake iliyogharimu Sh8.2 bilioni, Dk
Kashililah alisema viti vipya 678 vilivyofungwa kwenye ukumbi huo vimegharimu takribani
Dola za Marekani milioni moja (sawa na Sh1.6 bilioni) pamoja na gharama za
usafiri.
Alisema
gharama nyingine zimetokana na marekebisho ya mfumo wa sauti ambao ulikuwa
ukilalamikiwa na wabunge kutokana na kutosikika vizuri kwa baadhi ya vipaza
sauti.
Dk
Kashililah alisema ukarabati huo umehusisha, mfumo mpya unaotumia teknolojia ya
dijiti na kuboresha mitambo ya Idara ya Kuhifadhia ya Kumbukumbu Rasmi za Bunge
ili iweze kuhimili idadi ya wabunge hao zaidi ya 600.
Alisema
gharama nyingine zimetokana na ukarabati wa mifumo ya kuimarisha usalama pamoja
na kuweka vioo visivyopenya risasi katika baadhi ya kumbi.
Alisema
fedha nyingine zimetumika kukarabati paa la Ukumbi wa Bunge ambalo lilikuwa
linavuja.
Pia fedha hizo
zimetumika kurekebisha mitambo ya kufua umeme, maji, kuzima moto na viyoyozi na
kumalizia ujenzi wa jengo ambalo litakuwa likitumika kwa ajili ya sehemu ya
mazoezi, benki na ofisi za wabunge zaidi 100.
Dk
Kashililah alisema kiasi hicho kimetumika kwa ajili ya kununua samani za ofisi
za wabunge na kuongeza eneo la mgawaha na kuboresha miundombinu kwa ajili ya
watu wenye ulemavu.
Alisema
fedha zote zilizotumika katika ukarabati huo zimetokana na bajeti ya mipango ya
maendeleo iliyopitishwa na Bunge mwaka jana na kwamba si jambo geni huku
akisema kazi zote zimefanywa kwa mara moja.
Ratiba
ya Bunge la Katiba,Kwa upande wa ratiba ya Bunge la Katiba, Dk Kashililah
alisema litaanza shughuli zake rasmi kesho kwa kusomwa kwa tangazo la kuitishwa
kwa Bunge Maalumu la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Siku
hiyo pia kutafanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa muda ambaye kazi yake kubwa
itakuwa ni kuandaa kanuni za Bunge Maalumu la Katiba ambalo litakuwa na wajumbe
629.
Alisema
baada ya kupatikana kwa kanuni, Ijumaa kutafanyika uchaguzi wa mwenyekiti na
makamu wake kwa kuzingatia sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa mwaka
jana.
Alidokeza
kwa kusema pia kuwa wateuliwa, Katibu na msaidizi wake wa Bunge hilo na kwa
mujibu sheria hiyo, ataanza kazi baada ya kuapishwa na Rais na baada ya
kuapishwa naye atamwapisha mwenyekiti wa Bunge hilo.
Baada ya
mwenyekiti kuapishwa, atawalisha kiapo wajumbe wengine wa Bunge hilo, kazi
ambayo itafanyika kwa siku tatu hadi Jumatatu asubuhi na mchana wake, Rais
Kikwete atalizindua rasmi.
Source
mwananchi
0 comments:
Post a Comment