Na Baraka
Mpenja , Dar es salaam
KINYANG`ANYIRO
cha ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014, bado kinabaki
kuwa kitendawili kwa timu zilizopo juu katika msimamo.
Sare ya bao 1-1
jana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baina ya vinara Azam fc dhidi ya Yanga
imezidi kuweka mazingira magumu kwa mabingwa watetezi, Young
African.
Katika mchezo huo
uliovuta hisia za mashabiki, Yanga walikuwa wa kwanza kufunga bao kipindi cha
kwanza kupitia kwa Didier Kavumbagu, lakini Azam fc walisawazisha dakika za lala
salama kupitia kwa kinda, Kevin Friday.
Hiyo ilikuwa
mechi ya 19 kwa Yanga, wakati kwa Azam fc ilikuwa ya 20, huku wakijikusanyia
pointi 44, wakati Wanajangwani wakivuna pointi 40 katika nafasi ya
pili.
Yanga SC
wamebakiza mechi 7, wakati Azam fc wamebakiza mitanange 6.
Wikiendi hii timu
zote zitashuka dimbani. Yanga watasafiri mpaka mkoani Tabora kuwafuata maafande
wa Rhino Rangers, wakati jumapili machi 23, Azam fc watawakaribisha JKT Oljoro,
uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Rhino Rangers
ndio wanaoburuza mkia katika msimamo wakiwa wameshacheza mechi 21 na
kujikusanyia pointi 13 tu kibindoni.
Kwa asilimia
kubwa, maafande hawa wa Tabora, wameshachungulia kushuka daraja na inawezekana
hakuna muujiza wa kubaki ligi kuu msimu huu kwasababu ya mazingira
yao.
Mchezo dhidi ya
Yanga utakuwa mkali endapo bado Rhino wanahitaji ushindi.
Lakini imani yao
imeshuka na wanacheza bora liende na wameshapoteza matumanini ya kuendelea
kucheza ligi kuu.
Pointi 13 kwa
mechi 21 ni chache sana, zinahitajika nguvu za ziada kushinda mechi zote 5
walizobakiza, hapo sasa tunaweza kuzungumza mengine.
Yanga wataingia
uwanjani wakiwa ma matokeo ya sare ya jana na suluhu ya Mtibwa Sugar wiki
iliyopita uwanja wa Jamhuri.
Yanga sc
hawajafanya vizuri mechi zao mbili tangu watolewe na Al Ahly ligi ya mabingwa
kwa penati 4-3, machi 9 mwaka huu, jijini Alexndria, hivyo hawana cha kuwaza
zaidi ya ushindi.
Kama watashindwa
kupata ushindi katika mchezo huo, watakuwa wanazidi kuweka rehani ubingwa wao
msimu huu.
Kwa maana hiyo,
kocha mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm lazima awaeleze vijana wake umuhimu wa
mechi ya jumamosi endapo wanahitaji ketetea taji lao.
Wakati Yanga
wakiwa kwenye mawazo mazito juu ya mchezo huo, wapinzani wao, Azam fc watakuwa
wanasubiria matokeo ili kujipanga kwa mchezo wa kesho yake.
JKT Oljoro
waliopoteza matumanini ya kusalia ligi kuu msimu , wataingia kuwavaa Azam fc
ambao hawajapoteza mchezo mpaka sasa kwa lengo la kutafuta pointi
tatu.
Mechi za karibuni
zinaonesha kuwa Azam fc wamekuwa bora zaidi katika uwanja wao kwasababu
wanagawa dozi kubwa kwa wapinzani.
Mechi iliyopita
waliwafunga Coastal Union mabao 4-0, hivyo JKT Oljoro wasipokuwa makini
watachezea kipigo.
Endapo Azam fc
watashinda mechi hiyo, watazidi kujikita zaidi kileleni, nao Yanga wakishinda
watandelea kuwa wa pili.
Matokeo ya sare
au suluhu hayatakuwa mazuri kwa Yanga, kwasababu Mbeya City waliopo nafasi ya
tatu nao watacheza na JKT Ruvu jumamosi uwanja wa Chamazi.
Kama Yanga
hawatashinda na Mbeya City wakapata matokeo ya ushindi, basi Yanga watashuka
nafasi ya tatu.
Hata kama watatoa
sare au suluhu mjini Tabora, bado Yanga watabaki nafasi ya tatu, kwani Mbeya
City watakuwa wamefikisha pointi 42, Yanga 41.
Kama Yanga
watashinda na Mbeya City watashinda, basi nafasi za pili na tatu zitabaki kama
zilivyo.
Matokeo yoyote ya
Yanga na Mbeya City hayatakuwa na athari kwa Azam fc katika nafasi ya kwanza,
isipokuwa watasogelewa kwa pointi.
Wakati Yanga na
Azam fc wakichunao vikali kusaka ubingwa, mechi zilizosalia kwa timu zote ni
kama zifuatazo;
Yanga wamebakiza
mechi dhidi ya Rhino Rangers itakayochezwa machi 22 mwaka huu uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Baada ya hapo
atakuwa na mechi dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Taifa.
Ugumu wa mechi
hizi mbili unatokana na mazingira ya Prisons na Rhino kwa sasa.
Hawataki kushuka
daraja, zaidi Prisons wamedhamiria kubakia lihi kuu kuliko Rhino wanaoonekana
kukata tamaa.
Haitakuwa kazi
nyepesi kwa Yanga kuwafunga wajelajela hao uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam.
Mechi nyingine
zilizosalia kwa Yanga ni dhidi ya Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani
Tanga.
Hii pia itakuwa
na changamoto kubwa kwasababu Mgambo wanajinusuru kushuka daraja msimu
huu.
Pia Yanga
wamebakiza mechi dhidi ya Kager Sugar, Uwanja wa Taifa, mechi dhidi ya JKT
Oljoro, jijini Arusha, mechi na JKT Ruvu uwanja wa Taifa.
April 19 mwaka
huu Yanga watafunga msimu kwa kuvaana na Simba sc uwanja wa
Taifa.
Katika mechi saba
zilizosalia kwa Yanga, mechi mbili pekee ndizo atakutana na timu zilizopo salama
msimu huu na zinahitaji nafasi nne za juu.
Kagera Sugar
mpaka sasa wana uhakika wa kusalia ligi kuu pamoja na Simba sc ambao wanasaka
nafasi za juu.
Mechi nyingine
zote, Yanga atakutana na timu zinazopambana kukwepa mkasi wa kushuka daraja.
Hivyo lazima ajiandae kwa nguvu zote kwasababu kukamiana
kutakuwepo.
Kila timu
inahitaji kupata ushindi bila kujali inakutana na timu kubwa au
ndogo.
Kocha wa Yanga ,
Mholanzi, Hans Van Der Pluijm akisaidiwa na Charles Mkwasa wanahitaji kutuliza
sana akili zao kuelekea mechi hizo.
Azam fc amebakiza
mechi sita ambazo ni dhidi ya JKT Oljoro, Mgambo, Ruvu shooting, JKT Ruvu, Mbeya
City na Simba sc.
Mechi dhidi
yaMbeya City itakayopigwa sokoine Mbeya, itakuwa ngumu zaidi kwa Azam fc
kulingana na rekodi ya Mbeya City katika uwanja wake.
Mbeya City
hawajawahi kufungwa kwao, hivyo lazima Azam fc wajiandae kama wanataka kuvunja
rekodi hii.
Pia Mbeya City
wanasaka ubingwa wa kwanza kama ilivyo kwa Azam fc. Tofauti ni umri katika ligi.
Azam fc waliingia 2008/2009, Mbeya City waliingia 2013/2014.
Azam fc
ameshakuwa makamu bingwa kwa zaidi ya misimu miwili, wakati Mbeya City ndio
kwanza wanaanza kutafuta mafanikio.
Mechi hii itakuwa
ngumu kwa timu zote mbili, matokeo yatategemea jinsi makocha wote wawili, Juma
Mwambusi wa Mbeya City na Mcameroon, Joseph Marius Omog wa Azam fc
wamejipangaje.
Pia mechi dhidi
ya Simba sc itakuwa mlima mwingine kwa Azam fc kwasababu Simba hawatakuwa na
chakupoteza zaidi ya kusaka ushindi.
Kwa mazingira ya
mechi za Azam fc, itakuwa ngumu kwake kupata ushindi kwenye baadhi ya mechi
kwasababu wapinzani wake wanahitaji kujiweka vizuri katika
msimamo.
Simba na Mbeya
City wanawania nafasi za juu. Ruvu Shhoting anatafuta nafasi nzuri
pia.
Mgambo, JKT Ruvu,
JKT Oljoro wapo katika hatihati ya kukwepa kushuka daraja, hivyo mechi zao
zitakuwa ngumu zaidi kutokana na kukutana na timu ambayo inaongoza
ligi.
Haitakuwa kazi
nyepesi kwa Azam fc kuibuka na ushindi katika mechi hizi, lakini kama
watajiandaa vizuri basi wataweza kuvuna ushindi na kujihakikishia kutwaa ubingwa
msimu huu.
Ligi ya mwaka huu
imekuwa na changamoto kubwa kutokana na timu kubwa za Simba na Yaga kushindwa
kufua dafu kwa Azam fc na Mbeya City.
Misimu ya nyuma,
mpaka sasa ilikuwa rahisi kubashiri bingwa, na wakati mwingine timu ilikuwa
inatangaza ubingwa kabla ya mechi tatu au nne.
Kwa msimu huu
jambo hilo limebaki kuwa ndoto, ubingwa utaonekana mechi za mwisho, kwani mpaka
sasa mbio bado zipo wazi kwa klabu zaidi ya moja.
Katika soka, hii
ni hatua nzuri kwasababu inadhirisha zimekuweo timu zaidi ya mbili zenye ubora
wa juu, tofauti na miaka ya nyuma iliyokuwa na ufalme wa Simba na Yanga
src
shaffihdaudA

0 comments:
Post a Comment