Mfumo wa awali kuhusu Makamu wa Rais urejeshwe
KWANZA nampongeza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba
na Tume yake kwa kazi nzuri waliyofanya katika mazingira magumu. Inasikitisha
kusikia baadhi ya wanasiasa wakimjadili mtu badala ya kujadili hoja yenyewe.
Niseme hao wamefilisika kimawazo?
Ugomvi ni juu ya pendekezo la serikali tatu. Wakati Muungano ulipokuwa
unapingwa na kunyofolewa mbona hawakujitokeza kujibu hoja za wapinzani wa
Muungano? Walikuwa wapi? Ukimya wao sio ishara ya kuwaunga mkono wapinzani hao?
Je, walitaka Jaji Warioba atumie mabavu kama dikteta kwenda kinyume cha maoni
ya wananchi na wenzake katika Tume? Hiyo ndiyo demokrasia?
Pili, baada ya hayo, niseme pia kwamba binadamu hawezi kuwa mkamilifu
katika kutenda au kuamua mambo. Upo uwezekano pakawepo na upungufu na hivyo
kukawepo nafasi ya kufanya masahihisho na kuboresha. Katika rasimu hii ya pili
naona ina sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni maoni ya wananchi ambayo yameandikwa
katika mfumo wa kisheria. Sehemu ya pili, ni maoni ya Tume yenyewe.
Sehemu ya tatu ni baadhi ya mambo yaliyo katika Katiba ya sasa. Sitaingia
katika uchambuzi wa maeneo hayo. Hata hivyo niseme ni muhimu kuheshimu maoni ya
wananchi hata kama mtu hayataki na kama kuna uwezekano wa kuyaimarisha basi
yaimarishwe. Lakini pia kwa nia ya kuboresha yale ya msingi isiwe haramu kuwa
na mawazo tofauti na yale ya Tume yenyewe. Kwa mfano kuhusu orodha ya mambo ya
Muungano, nafasi ya Makamu wa Rais, utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais kabla ya
kumaliza kipindi chake au wakati hayupo, utaratibu wa kupata wagombea urais au
ubunge ili kupata wagombea wenye sifa, kumshtaki Rais, utaratibu wa kubadilisha
Katiba na mengineyo. Naomba nitoe maoni yangu kwenye maeneo hayo ambayo lengo
lake ni kuboresha na sio kuathiri msingi.
Mambo ya Muungano (ibara ya 63)
Ili kupata Serikali ya Muungano yenye nguvu na mamlaka ya kutosha, ipo haja
ya kuongeza orodha ya mambo ya Muungano:
Yanayoweza kuongezwa ni masuala ya anga; mawasiliano; usafiri wa baharini.
Maeneo hayo yanahusika na ulinzi na usalama wa taifa, hivyo napendekeza mambo
hayo yawekwe chini ya mamlaka ya Serikali ya Muungano. Maeneo mengine ambayo ni
muhimu yakadhibitiwa na Serikali ya Muungano ni misaada, mikopo (ibara
229) na madeni ya nje, lengo ni kuiwezesha Serikali ya Muungano kutimiza
ipasavyo wajibu wake mkuu wa kulinda Jamhuri ya Muungano isichezewe na maadui
wa nje au wa ndani.
Nchi inaweza kuuzwa kutokana na misaada mikubwa au mikopo iliyokidhiri
kiasi cha kushindwa kulipa. Kuna nchi zilizopoteza uhuru wao kwa sababu hizo.
Au nchi kuyumbishwa kwa sababu hiyo. Na nchi yetu imeonja hayo tulipotofautiana
na “Wakubwa”. Pia tunaona jinsi baadhi ya nchi zilizoendelea zinavyoyumba
kiuchumi kwa sababu ya kusongwa na madeni makubwa ya nje na sera bovu za uchumi
, kwa mfano Ugiriki. Hivyo kama mshirika mmoja wa Muungano atafanya madudu huko
madhara yake yataathiri taifa zima.
Bila shaka katika kutumia mamlaka hayo, Serikali ya Muungano sharti
ishirikishe serikali za nchi washirika.
Wajibu wa kulinda Muungano
Tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa suala la jinsi ya kumpata
Makamu wa Rais wa Jamhuri lilipasua vichwa vya watu. Mwishowe ikakubalika dhana
ya mgombea mwenza wa mgombea kiti cha urais ambaye atakuwa Makamu wa Rais wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uamuzi huu pamoja na sababu
zake zilizotolewa, uliacha pengo.
Rais wa Serikali ya Zanzibar hakuwa kiungo tena cha Muungano wa nchi mbili
zilizoungana wala hakuwa tena na dhamana ya kuulinda Muungano kwa kiwango
kilichostahili. Yaliyofuata baadaye huko Zanzibar ni hayo tunayoyashuhudia sasa
hata kufikia hatua ya kupitisha Katiba yao ambayo imeingilia mamlaka ya
Serikali ya Muungano kwenye maeneo mbalimbali ya utendaji na sera. Pia
upinzani dhidi ya Muungano ukaongezeka kwa kasi ukisimamiwa na Viongozi wa juu
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Maridhiano yaliyotokea kati ya Chama cha
Wananchi (CUF) na Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na yaliyofuatana nayo,
yaliwezekana kwa sababu kiungo muhimu cha Muungano kutoka Zanzibar kilikosekana
na kimekosekana. Iliwezekana kumvua madaraka Makamu wa Kwanza wa Rais, Aboud
Jumbe kwa sababu kwa nafasi yake, alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM akiwa na wajibu mkuu wa wajibu wake
wa kuilinda Katiba ya Muungano. Lakini alikuwa anafanya mambo ya kichini chini
ya kudhoofisha Muungano mpaka alipofichuliwa.
Zile sababu zilizotumiwa kubadilisha kipengee hiki zilijengwa juu ya hofu
ya kuwa “itakuwaje kama katika uchaguzi Rais na Makamu wake watatoka
katika vyama tofauti- watafanyaje kazi kwa pamoja – huyu ni CUF na huyu ni
CCM?” Kumbe duniani humu kuna serikali za mseto na serikali ya umoja wa taifa.
Ili kuimarisha uwajibikaji na kuimarisha Jamhuri ya Muungano napendekeza mfumo
uliokuwapo kuhusu nafasi ya Makamu wa Rais kabla ya kuingia kwa mfumo wa vyama
vingi vya siasa urejeshwe.
Utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais kabla
Pendekezo kwamba; “Makamu wa Rais ataapishwa kushika madaraka ya Rais kwa
muda uliobakia katika kipindi cha miaka mitano …”, kwa maoni yangu, halifai
kwani linatoa nafasi kwa Ibilisi au adui wa nje au wa ndani kufanya njama za
kumwondoa Rais aliye madarakani ili Makamu wake achukue nafasi hiyo. Kama
inatokea na imekwishatoa mtoto wa mfalme kumpindua baba yake ili achukue ufalme
wake, inawezekana kutokea pia kwa hili na kwa urahisi zaidi. Napendekeza kwamba
nafasi ya Rais ikitokea kuwa wazi achaguliwe mwingine katika muda usiozidi
miezi mitatu kama ilivyo katika Katiba ya sasa.
Utekelezaji majukumu ya Rais asipokuwapo
Mapendekezo kwamba; “Ikitokea nafasi ya madaraka ya Rais iko wazi kutokana
na kazi… na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo wa wafuatao, kwa
kufuata orodha kama ilivyopangwa.
Napendekeza kwamba nafasi ya Rais wakati hayupo isishikwe na mtu ambaye
hakuchaguliwa na wananchi. Kufanya hivyo ni kudhalilisha nafasi hiyo. Hivyo kwa
kuwa mawaziri hawatateuliwa kutoka miongoni wa wabunge, waziri yeyote
hana sifa ya kushika nafasi hiyo.
KUHUSU SIFA ZA KUCHAGULIWA KUWA MGOMBEA NAFASI YA URAIS AU
UBUNGE (IBARA YA 79 NA 125):
Kwa sasa vyama ndivyo vinavyopendekeza- kwa kweli kuteua mgombea. Kumbe
baadhi ya walioteuliwa kugombea wasingechaguliwa kama wapiga kura wangewajua.
Propoganda za vyama na mashabiki ndizo zinazotawala. Matokeo yake Taifa
linapata viongozi wabovu na serikali dhaifu. Napendekeza kwamba pawepo na
chombo cha kuchuja na kuhahiki sifa za wagombea waliopendekezwa na vyama. Kiwe
na mamlaka ya kuyakataa na kuagiza vyama vipendekeze wengine au mwingine. Tume
ya uchaguzi ipewe mamlaka hayo. Katika kutekeleza wajibu huu Tume itaongozwa na
miiko ya uongozi iliyoorodheshwa katika Katiba hii. Zipo nchi
nyingine zenye utaratibu huo wa kuchuja. Bila kuwa na chombo kama hicho sifa
hizo zitabaki kwenye makaratasi na mambo yataendelea kama kawaida tulioizoea na
Taifa litaendelea kupata viongozi wabovu.
BUNGE KUMSHITAKI RAIS (IBARA YA 88 (6) (12)): Ni maoni
yangu kwamba kiwango kilichopendekezwa cha 75% ya kura za Wabunge kwa
ajili ya kuunda Kamati ya Uchunguzi na cha kumwondoa
Rais ni cha juu mno. Kwa nini asilimia zaidi ya 50 isitoshe
kwa ajili ya kuunda Kamati hiyo na asilimia 66 (theluthi mbili) isitoshe
kumwondoa?. Zaidi ya kiwango hicho ni “KULINDANA”.
Pia katiba itamke Rais au kiongozi aliyeondolewa madarakani asistahili
kulipwa mafao ya uzeeni – pensheni - kama ilivyo kwa watumishi wengine wa
umma wanaofukuzwa kazi..
_ UTARATIBU WA KUBADILISHA KATIBA (IBARA YA 118). Kwa hili
tuongozwe pia na uzoefu tuliokwishapata na uzito wa Katiba iliyopitishwa na
wananchi. Utararibu wa kubadilisha katiba usiwe rahisi kama huu uliyopendekezwa
ambao ndiyo unaotumika sasa. Utaratibu huu ndio ulioiwezesha Chama tawala kwa
kutumia wingi wa wabunge wake Bungeni kufuta haki ya raia binafsi
kugombea Urais au Ubunge bila ya kuteuliwa na chama cha siasa. Tusiruhusu
utaratibu huu wa kubadilisha Katiba uendelee. Napendekeza:
Theluthi mbili wa wabunge kutoka Tanganyika na theluthi mbili kutoka
Zanzbar zitahitajika kama ilivyo sasa, na; Theluthi mbili ya wabunge wa
upinzani – hawa wanawakilisha wananchi waliowachagua; Kama mabadiliko
yanayokusudiwa ni makubwa Ibara 119 iliyopendekezwa naunga mkono.
KUUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO - UKUBWA
WA BUNGE (IBARA YA 113) (na utaratibu wa kuchagua Wabunge):
Ibara hii inahitaji uchambuzi wa kina, isije ikashindikana kuitekeleza. Naona
Jimbo la uchaguzi eneo lake litakuwa kubwa mno hata kufanya kazi ya wagombea
kufanya kampeni kuwa ngumu na yenye gharama kubwa. Yapo pia maswali
yakujiuliza: Ilani ya uchaguzi ya chama au mgombea itakuwa na sera za aina gani
kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje nk. ili kuwashawishi wapiga
kura wapigiwe kura? Tume ingeangalia uwezekano wa Mabunge ya Nchi Washirika
kuchagua wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kama inavyofanyika sasa kwa
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ila Rais atachaguliwa na wananchi.
Napendekeza iwe hivyo.
MAJUKUMU YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI (IBARA 196 (3)) – Kwamba
“Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi atatekeleza majukumu yake
kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa umma ….”.
Mkurugenzi asilazimishwe kutumia watumishi wa umma kama ilivyo sasa. Ushahidi
upo unaoonyesha kwamba watumishi hao wanajikuta wanatumikia mabwana
wawili- Tume kwa upande mmoja na mwajiri wake kwa upande wa pili ambaye anataka
matakwa yake yatekelezwe na hivyo kupotosha haki! Napendekeza Tume iwezeshwe
kuajiri/ kuteua watumishi wake ambao watawajibika kwake tu.
11. VYANZO VYA MAPATO YA SERIKALI YA MUUNGANO . (IBARA YA
231) :
1). Pendekezo hili, kwa maoni yangu, litazaa Serikali dhaifu na kuweka Jamhuri
ya Muungano kama kivuli. Ni Serikali gani ambayo haina mamlaka ya kutoza kodi
wananchi wake ili iweze kuwatumikia ipasavyo? Tunataka Serikali ya Muungano
yenye nguvu. Nguvu hii ni pamoja na uwezo wa kupata mapato ya kutosha ya
kuendesha Serikali ya Muungano. Mapato hayo yachangiwe na kila mwananchi mwenye
uwezo wa kulipa kodi na kila taasisi inayolipa kodi kwa mujibu wa sheria. Kwa
utaratibu wa sasa wananchi wanalipa kodi inayoendesha shughuli za Muungano na
shughuli za Tanzania Bara na Zanzibar.
Napendekeza pawepo na Chombo cha Muungano kitakachoshirikisha kikamilifu
Washirika kitakachosimamia kodi. Pawepo na vigezo vya kugawa kodi inayokusanywa
kati ya Serikali ya Muungano na Nchi Washirika. Vigezo hivyo vizingatie ukubwa
wa Nchi Mshirika na idadi ya wananchi pamoja na vigezo vingine vinavyoweza
kubuniwa na kukubalika. Tunaweza kujifunza kutoka nchi nyingine.
Utaratibu huu hautasababisha ongezeko la kodi kwa ajili ya shughuli za
Serikali ya Muungano.
Hata kama ushuru wa bidhaa ungetosha (Ibara 231 (a) - hiyo ni
kuitenga Serikali na wananchi wake waione kama si yao kwa sababu haigusi mifuko
yao. Kwa maoni yangu, Serikali inayoendeshwa na “indirect Tax” na
inayolipwa na idadi ndogo ya wananchi ambao wala hawana habari na kodi
hiyo, haiwezi kuwa ni Serikali ya wananchi , wala wananchi
hawatakuwa na nguvu ya kuihoji Serikali. Kodi yao ndiyo inayowapa nguvu ya
kuihoji Serikali.
2). Pendekezo lililotolewa la Nchi Washirika kuchangia -231 (c) -
halifai. Itakuwaje na ni hatua gani Serikali ya Muungano itakayochukua kama
Mshirika mmoja hachangi kwa sababu mbali mbali? Na ni vigezo gani
vitatumika kuchangisha? Kwani hali ya sasa jkoje? Je, wananchi au wawakilishi
wao wanajua kama Zanzibar inachangia kiasi gani kwenye bajeti ya kuendesha
Mambo ya Muungano? Mapato yapatikane moja kwa moja kutoka vyanzo vyake halisi.
Ndiyo kazi itakayofanywa na chombo kilichopendekezwa hapo juu
KUHUSU sifa za kuchaguliwa kuwa mgombea nafasi ya urais au Bunge (ibara ya
79 na. 125), kwa sasa vyama ndivyo vinavyopendekeza- kwa kweli kuteua mgombea.
Kumbe baadhi ya walioteuliwa kugombea wasingechaguliwa kama wapiga kura
wangewajua. Propoganda za vyama na mashabiki ndizo zinazotawala. Matokeo
yake taifa linapata viongozi wabovu na serikali dhaifu.
Napendekeza kwamba pawepo na chombo cha kuchuja na kuhahikiki sifa za
wagombea waliopendekezwa na vyama. Kiwe na mamlaka ya kuyakataa na kuagiza
vyama vipendekeze wengine au mwingine. Tume ya Uchaguzi ipewe mamlaka hayo.
Katika kutekeleza wajibu huu, tume itaongozwa na miiko ya uongozi
iliyoorodheshwa katika Katiba hii.
Zipo nchi nyingine zenye utaratibu huo wa kuchuja. Bila kuwa na chombo kama
hicho sifa hizo zitabaki kwenye makaratasi na mambo yataendelea kama kawaida
tuliyoizoea na taifa litaendelea kupata viongozi wabovu.
Bunge kumshitaki Rais
Ni maoni yangu kwamba kiwango kilichopendekezwa cha asilimia 75 ya kura za
wabunge kwa ajili ya kuunda Kamati ya Uchunguzi na cha kumwondoa Rais ni cha
juu mno. Kwa nini asilimia zaidi ya 50 isitoshe kwa ajili ya kuunda kamati hiyo
na asilimia 66 (theluthi mbili) isitoshe kumwondoaZaidi ya kiwango hicho ni
“KULINDANA”.
Pia Katiba itamke Rais au kiongozi aliyeondolewa madarakani asistahili
kulipwa mafao ya uzeeni – pensheni - kama ilivyo kwa watumishi wengine wa
umma wanaofukuzwa kazi.
Utaratibu wa kubadili Katiba
Kwa hili tuongozwe pia na uzoefu tuliokwishapata na uzito wa Katiba
iliyopitishwa na wananchi. Utararibu wa kubadilisha Katiba usiwe rahisi kama
huu uliopendekezwa, ambao ndiyo unaotumika sasa. Utaratibu huu ndio
uliokiwezesha chama tawala kwa kutumia wingi wa wabunge wake bungeni kufuta
haki ya raia binafsi kugombea urais au ubunge bila ya kuteuliwa na chama cha
siasa. Tusiruhusu utaratibu huu wa kubadilisha Katiba uendelee.
Napendekeza kwanza, theluthi mbili wa wabunge kutoka Tanganyika na theluthi
mbili kutoka Zanzibar zitahitajika kama ilivyo sasa na pili; theluthi mbili ya
wabunge wa upinzani – hawa wanawakilisha wananchi waliowachagua, tatu; kama
mabadiliko yanayokusudiwa ni makubwa ibara 119 iliyopendekezwa naunga mkono.
Kuundwa kwa Bunge la Jamhuri
Ibara ya 113 inahitaji uchambuzi wa kina, isije ikashindikana kuitekeleza.
Naona jimbo la uchaguzi eneo lake litakuwa kubwa mno hata kufanya kazi ya
wagombea kufanya kampeni kuwa ngumu na yenye gharama kubwa. Yapo pia maswali ya
kujiuliza: Ilani ya uchaguzi ya chama au mgombea itakuwa na sera za aina gani
kuhusu masuala ya ulinzi na usalama, mambo ya nje na mengineyo kama hayo ili
kuwashawishi wapiga kura wapige kuraTume ingeangalia uwezekano wa mabunge ya
nchi washirika kuchagua wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kama
inavyofanyika sasa kwa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ila Rais
atachaguliwa na wananchi. Napendekeza iwe hivyo.
Majukumu ya Mkurugenzi wa uchaguzi
Majukumu ya mkurugenzi wa uchaguzi (ibara ya 196; -3) – kwamba “Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa na
watendaji ambao ni watumishi wa umma ….” Mkurugenzi asilazimishwe kutumia
watumishi wa umma kama ilivyo sasa. Ushahidi upo unaoonyesha kwamba watumishi
hao wanajikuta wanatumikia mabwana wawili- Tume kwa upande mmoja na mwajiri
wake kwa upande wa pili ambaye anataka matakwa yake yatekelezwe na hivyo
kupotosha haki! Napendekeza Tume iwezeshwe kuajiri au kuteua watumishi wake
ambao watawajibika kwake tu.
Vyanzo vya mapato ya serikali ya Muungano
Katika vyanzo vya mapato ya serikali ya Muungano (ibara ya 231) kwanza;
pendekezo hili, kwa maoni yangu, litazaa serikali dhaifu na kuweka Jamhuri ya
Muungano kama kivuli. Ni serikali gani ambayo haina mamlaka ya kutoza kodi
wananchi wake ili iweze kuwatumikia ipasavyo
Tunataka Serikali ya Muungano yenye nguvu. Nguvu hii ni pamoja na uwezo wa
kupata mapato ya kutosha ya kuendesha Serikali ya Muungano. Mapato hayo
yachangiwe na kila mwananchi mwenye uwezo wa kulipa kodi na kila taasisi
inayolipa kodi kwa mujibu wa sheria. Kwa utaratibu wa sasa wananchi wanalipa
kodi inayoendesha shughuli za Muungano na shughuli za Tanzania Bara na
Zanzibar.
Napendekeza pawepo na Chombo cha Muungano kitakachoshirikisha kikamilifu
Washirika kitakachosimamia kodi. Pawepo na vigezo vya kugawa kodi inayokusanywa
kati ya Serikali ya Muungano na Nchi Washirika. Vigezo hivyo vizingatie ukubwa
wa Nchi Mshirika na idadi ya wananchi pamoja na vigezo vingine vinavyoweza
kubuniwa na kukubalika. Tunaweza kujifunza kutoka nchi nyingine.
Utaratibu huu hautasababisha ongezeko la kodi kwa ajili ya shughuli za Serikali
ya Muungano.
Hata kama ushuru wa bidhaa ungetosha (Ibara 231 (a) - hiyo ni
kuitenga Serikali na wananchi wake waione kama si yao kwa sababu haigusi mifuko
yao. Kwa maoni yangu, Serikali inayoendeshwa na “indirect Tax” na
inayolipwa na idadi ndogo ya wananchi ambao wala hawana habari na kodi
hiyo, haiwezi kuwa ni Serikali ya wananchi , wala wananchi
hawatakuwa na nguvu ya kuihoji Serikali. Kodi yao ndiyo inayowapa nguvu ya
kuihoji Serikali.
Pendekezo lililotolewa la Nchi Washirika kuchangia -231 (c) - halifai.
Itakuwaje na ni hatua gani Serikali ya Muungano itakayochukua kama Mshirika
mmoja hachangi kwa sababu mbali mbaliNa ni vigezo gani vitatumika
kuchangishaKwani hali ya sasa ikojeJe, wananchi au wawakilishi wao wanajua kama
Zanzibar inachangia kiasi gani kwenye bajeti ya kuendesha Mambo ya
MuunganoMapato yapatikane moja kwa moja kutoka vyanzo vyake halisi. Ndiyo kazi
itakayofanywa na chombo kilichopendekezwa hapo juu.
src
Raia mwema
0 comments:
Post a Comment