DENI la taifa limeongezeka kwa kasi kubwa, hali ambayo inatishia ustawi wa taifa kama halitasimamiwa kwa umakini na haraka. Hotuba ya Waziri wa Fedha (ya bajeti 2014/2015) inaonesha kwamba hadi kufikia Machi 2014, Deni la Taifa lilifikia shilingi trilioni 30.563 ikilinganishwa na shilingi trilioni 23.674 la Machi 2013. Hilo ni ongezeko la takribani trilioni 7 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 29 kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.
Hili ongezeko la mikopo ya takribani shilingi trilioni 7 kwa mwaka mmoja tu, halijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Ongezeko hili la takribani trilioni 7 ni sawa na bajeti nzima (full budget) ya mwaka 2008/9 ambayo ilikuwa ni shilingi trilioni 6.839. Ikumbukwe kuwa mwaka 2008/9 ni miaka mitano tu iliyopita. Ukopaji wa namna hii unatishia uchumi na usalama wa nchi.
Kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu na hotuba za bajeti za miaka iliyopita za Mawaziri wa Fedha, deni la Taifa limeongezeka kwa kasi kutoka shilingi trilioni 9.3 mwaka 2007/8 hadi shilingi trilioni 30.6 mwaka 2013/14. Hii ni wazi kuwa deni liliongezeka kwa kiasi cha shilingi trilioni 21.3. Serikali imelipa shilingi trilioni 4 na kufanya fedha zilizokopwa kuwa jumla ya shilingi trilioni 25.3 katika kipindi hicho cha miaka saba tu. Huu ni ukopaji hatarishi kwa uchumi wa taifa letu.
Licha ya deni hili kuwa hatarishi kwa uchumi wa Taifa, Serikali bado inatajaria kuongeza deni hilo kwa kukopa shilingi trilioni 4.3 kama ilivyoainishwa katika bajeti ya mwaka 2014/15.
Serikali imeonesha kushindwa kulipa deni hilo kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato, badala yake imekuwa ikikopa ili kulipa deni. Mfano hotuba ya bajeti ya mwaka 2014/15 imeonesha kuwa katika shilingi trilioni 1.8 zilizokopwa katika soko la ndani, zaidi ya shilingi trilioni 1.1 zilitumika kulipa madeni ya hati fungani wakati shilingi trilioni 0.69 tu ziliwekwa kwenye miradi ya maendeleo. Hiki ni kiashiria cha karibu sana kwa serikali kufilisika. Kukopa mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa ili kulipa mikopo yenye riba ndogo au kwa uendeshaji wa kawaida wa serikali au taasisi zake ni kiashiria cha kutosha kuainisha maamuzi yasiyo na uelewa wa kawaida sana wa utawala na usimamizi wa fedha (basic business and economic sense). Mikopo ya kibiashara hutafutwa kwa matumizi ya uwekezaji wenye lengo la uzalishaji.
Katika uchumi unaokuwa kwa wastani wa asilimia kati 6.5 na 7 kwa mwaka, ni vigumu sana kuweza kulipa deni la taifa linalokua kwa wastani wa asilimia kati ya 15 na 30 kwa mwaka. Bila kuwa na vyanzo vipya vya mapato au kusamehewa deni hili itakuwa vigumu sana kuweza kulipa deni hilo kikamilifu. Hii ni kwa sababu uwiano wa ukuaji wa uchumi hauendani na kasi ya ukuaji wa deni hata kidogo. Pamoja na upungufu wote huu, Serikali imeendelea kujitapa kuwa inakopesheka, na hivyo kuashiria kutokuwepo na hofu yeyote ya kukopa huku holela.
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa sehemu kubwa ya mikopo hii inakopwa katika soko la ndani. Hali hii imekuwa ikileta ushindani mkubwa kwa wananchi na wajasiriamali wanaotaka kukopa ili kukuza mitaji. Hali hii hufanya riba za mabenki kushindwa kushuka na hivyo kuwaathiri wakopaji na uchumi wa nchi kwa ujumla. Kwa maneno mengine, serikali imekuwa inazuia wajasiriamali wasikope kwa riba za bei nafuu, hivyo kufanya baadhi ya wanaokopa kwa riba zilizopo, ambazo ni kubwa kufilisiwa. Hali hii hurudisha biashara nyuma na inainyima serikali fursa ya kukuza uchumi na kukusanya mapato zaidi.
Mataifa mengi duniani yanakopa na yana madeni makubwa. Suala la msingi la kutofautisha nchi moja na nyingine ni kasi ya kukua kwa deni husika na matumizi ya mkopo huo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inauliza na kutaka majibu kutoka kwa Serikali matumizi ya fedha zilizokopwa na nchi yetu ndani ya miaka 7 ni yapi na yameleta maendeleo kiasi gani kwa Taifa ( value for money).
Kwa mujibu wa bei za soko kuhusu trekta ambazo serikali imeziidhinisha kuwa ziuzwe hapa nchini kwa ajili ya kilimo kupitia mradi wa Taifa wa Kilimo Kwanza, ni wastani wa shilingi milioni 30 kwa trekta moja lenye ubora wa hali ya juu. Endapo fedha zilizokopwa kwa miaka saba, shilingi Trilioni 25.3, zingetumika kuweka kipaumbele katika kilimo na kununua matrekta ya kisasa yenye ubora wa hali ya juu, ni dhahiri serikali ilikuwa na uwezo wa kununua matrekta 843,333. Kwa kuzingatia Kata tulizonazo hapa nchini (3000), Matrekta hayo yangeweza kugawiwa kwa kila kata kupata trekta 281. Hakika kama hili lingetendeka, Taifa letu lingekuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuzalisha chakula duniani.
Endapo fedha zilizokopwa kwa kipindi cha miaka saba zingetumiwa katika sekta ya elimu, kila mwanafunzi anayesoma kuanzia shule ya msingi hadi Chuo kikuu, angeweza kutengewa milioni mbili na laki tatu (sh. milioni 2.318) kwa ajili ya shule. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za sasa kuwa kuna jumla ya wanafunzi wanaokadiriwa asilimia 23 ya Watanzania wote, ambao ni takriban wanafunzi 10,350,000 katika shule zote za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya ualimu na vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini.
Je, fedha hizi zilizokopwa na ambazo zitaendelea kukopwa na kuleta mzigo mkubwa kwa Watanzania zimefanya nini? Kumekuwa na ukosefu wa taarifa za wazi kuhusu mikopo kwa serikali yetu. Kuendelea kukosa taarifa hizi ni kubariki mianya ya ubadhirifu na upotevu wa fedha za umma na kuendelea kubebesha watanzania mzigo wa kulipa bila kufahamu fedha hizo zimefanya kazi gani za maendeleo.
Ni wakati muafaka sasa kwa Bunge kutunga sheria ya bajeti haraka iwezekanavyo, pamoja na mambo mengine ili iweze kudhibiti ukopaji na matumizi ya mikopo ya serikali. Vile vile tunapendekeza katika sheria hiyo iwe lazima kwa serikali kupata kibali kutoka katika Bunge lako tukufu kabla ya kuweza kukopa. Hii inafanyika katika nchi nyingi duniani kama vile Marekani na Uingereza.
Lakini mbali na haya, hali serikalini si nzuri katika masuala ya uchumi na fedha na hasa kuhusu usimamizi au utekelezaji wa bajeti inayopitishwa na Bunge.
Inaonesha kwamba makadirio ya mapato ya mwaka unaoshia Juni 30, 2014 hayatafikiwa kwa kiasi cha asilmia 10. Inakadiriwa kiasi kitakachopatikana ni takriban Shilingi trilion 17 badala ya Shilingi trilioni 18.249. Hivyo lengo la la mapato ya Shilingi trilioni 19.853 katika bajeti ya mwaka 2014/15 haliendani na hali halisi (unrealistic) na hivyo itasababisha ukopaji zaidi ya ule uliowekwa kwenye bajeti. Na kwa hiyo, kwa pamoja wabunge wa upinzani bungeni imetubidi kupendekeza mfumo wa ukadiriaji wa mapato ya serikali uwe wa uhalisi (realsitic) kuliko ilivyo sasa.
Ili bajeti iweze kutekelezwa kwa ufanisi ni lazima ionyeshe madeni yatakayoingia mwaka mpya wa fedha (kama yapo) na namna ambavyo madeni hayo yatalipwa.
Katika hotuba ya bajeti kwa mwaka 2014/15 Serikali ilieleza bungeni namna ambavyo sekta mbalimbali za maendeleo zitagawiwa fedha lakini hatujaelezwa juu ya madeni ya kila sekta yenye jumla ya takribani shilingi trilioni mbili ambayo hayakulipwa katika bajeti ya 2013/14 yatakavyolipwa.
Kutokuonesha madeni hayo katika bajeti kutaifanya bajeti hii mpya isitekelezeke kama zingine zilizotangulia kwani tunajua kuwa fedha zitakazokusanywa zitalipia kwanza madeni hayo. Serikali itoe ufafanuzi wa jambo hili, kwamba madeni haya ni kiasi gani na namna ambavyo yatalipwa.
Matumizi ya magari ya anasa yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa. Karibu viongozi wote wa ngazi za Wakurungezi, Makamishna, Makatibu Wakuu, na Mawaziri wananunua na kutumia magari aina ya Toyota Landcruiser V8 (Mashangingi), licha ya kuwa thamani ya kila gari moja la aina hiyo ni zaidi ya shilingi milioni 280, pia gharama ya kuyaendesha ni ya ghali sana.
Hatua kali zinatakiwa kuchukuliwa kwa wale watumishi wa umma watakaobainika kufanya ubadhirifu au kujihusisha na rushwa wakati wa kufanya manunuzi ya umma. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kila mwaka hutoa taarifa za ubadhirifu lakini hakuna hatua zinazotangazwa kuchukuliwa na Serikali kuwawajibisha wahusika. Tabia hii inawavunja moyo walipa kodi waaminifu.
Tukiwa wazalendo wa nchi yetu, sote tunatakiwa kujiuliza maswali kwa nini hatutafikia malengo yaliyomo kweney dira ya taifa? Ni wazi majibu yatakuwa hatuna sera ya kuwezesha utekelezaji wa mpango, pili hatuna sera ya kupunguza matumizi yasio ya lazima. Aidha, mpaka sasa hakuna utashi ulio bayana wa serikali kufanyia kazi maswali haya.
Ni jambo lililo dhahiri kwa viongozi walio wengi, hufanya matumizi ya anasa na kulipana posho kubwa, wakati wananchi walio wengi hawapati huduma muhimu? Tunatakiwa kujiuliza, je kwa mwenendo tunaokwenda nao malengo haya yatafikiwa? Swali hili ni la msingi tukizingatia kwamba Mpango huu wa miaka mitano ni sehemu ya Dira ya Taifa ya 2025, ambayo inalenga kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye kipato cha uchumi wa kati (middle-income country). Dira ya Taifa ya 2025, inalenga kuiwezesha Tanzania kuwa na wastani wa kipato cha mwananchi (per capita income) cha Dola za Marekani 3,000 ifikapo 2025.
Wabunge wa upinzani bungeni kwa upande wetu tumeitaka Serikali kuweka wazi ni hatua gani hadi sasa zimefikiwa katika; kwanza kutekeleza mpango wa miaka mitano, pili kutekeleza Dira ya Taifa ya 2025 na tatu, nini mategemeo au matarajio ya nchi kiuchumi pindi muda huo utakapofika?
Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005 inasema; “Kukuza uchumi kwa kiwango cha zaidi ya asilimia kumi (10%) kwa mwaka ifikapo 2010 kutoka ukuaji wa sasa wa asilimia sita nukta saba (6.7%)” Pia “Kuanza kupunguza umaskini wa watu wetu kwa namna iliyo dhahiri”, haya yalikuwa ni malengo ya kufikia mwaka 2010, ambapo hadi sasa uchumi huijafikia asilimia 10. Aidha, asilimia 28.1 ya Watazania wote wanaishi chini ya mstari wa umaskini (below poverty line kwa takwimu za Benki ya Dunia za mwaka 2012), hii ni sawa na Watanzania milioni 12. Je, bajeti ya taifa inawezaje kutumika katika kupunguza umaskini?
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 cha utekelezaji wa Bajeti ya Serikali, inayoongozwa na CCM, haijafanikiwa kuwa na bajeti yenye uhalisia wa kupunguza umaskini wa Watanzania, kwani bajeti inayolenga kupunguza umaskini: mosi; ni ile ambayo inayolenga kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi, pili; ni ile ambayo inatengeneza ajira nyingi kwa wananchi wake, tatu; ni ile ambayo inakuza uwekezaji hasa wa ndani, nne; ni ile inayomfanya Mtanzania aweze kuweka akiba (savings).
Tano, ni ile ambayo inalenga kuinua maisha ya walio wengi ambao wako vijijini, sita; ni ile inayolenga uchumi wa nchi umilikiwe kwa asilimia iliyo kubwa na wananchi wake, saba; ni ile inayolenga kukuza ujasiriamali na vile vile ni ile inayokuza ulaji (increased consumption).
Wataalamu tunao, rasilimali tunazo, nia tunayo, ni kwa vipi tunashindwa? Ni vema sasa Serikali iliambie Bunge lako Tukufu nini kikwazo cha kuteleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano? Au ni hila za serikali iliyoko madarakani, kuwafanya Watanzania waendelee kuwa maskini kwa maslahi yao kisiasa?
Ushauri wetu wabunge wa upinzani bungeni, ni kwamba tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema, tuuungane pamoja kwa masilahi mapana ya nchi yetu ya kuwatoa Watanzania katika lindi hili la ufukara. Kwani Mwenyezi Mungu ametujali utajiri mkubwa wa rasilimali za kila aina , ili Tanzania pawe mahali salama pa kuishi na kukuza Utu wa Binadamu.
Matatizo ni mwegi, kwa mfano, kwa muda mrefu sasa suala la ajira kwa vijana limejadiliwa katika Bunge, lakini halijapatiwa bajeti ya kutosha. Ni jambo lililo wazi kwamba litaendelea kuwa ni tatizo kwa la Taifa na hatimae kuwa ni bomu linalosubiriwa kulipuka wakati wowote. Upo umuhimu wa kulitafutia ufumbuzi wa kibajeti kwani vijana ndiyo rasilimali kazi kuu kwa maendeleo ya taifa.
Inakadiriwa kwamba ajira kwenye sekta rasmi ni 1,352,559 na kati ya hizo asilimia 68.1 ni ajira katika sekta binafsi isiyo rasmi. Tafsiri yake ni kwamba ukichukua idadi ya watu millioni 24 wenye uwezo wa kufanya kazi, idadi yao kubwa wako kwenye sekta isiyo rasmi na wengine wengi hawana ajira. Swali je, Bajeti hii inawezaje kutumika katika kutengeneza ajira?
Kwa upande wetu, wabunge wa upinzani bungeni tumeitaka Serikali ishirikiane na sekta binafsi, ili kuweka mikakati ya kuwa na bajeti ambayo itaifanya sekta binafsi ipanuke na iweze kuongeza uwezo wake wa kuajiri.
Suala la mazingira bora kwa uwekezaji ni la muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote duniani, hususani kwa nchi zenye nia ya kukuza uchumi wake. Utekelezaji wa dhana hii unatakiwa uanzie serikalini na kwa mtu mmoja mmoja.
Ni vema Serikali ikatoa motisha na mazingira rafiki kuiwezesha sekta binafsi iweze kukua kwani ndiyo injini ya kukuza uchumi wetu na kuzalisha ajira nyingi kwa vijana wetu. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi ifanye upembuzi wa kina unaolenga miaka mitano au hata kumi ijayo ya namna ya kuweka sera (macroecnomic policies) ambazo zitakuwa ni kivutio kwa makampuni yaliyopo kuweza kukuza uwekezaji.
src
James Mbatia
raia mwema

0 comments:
Post a Comment