Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu
Serikali ya Israel imekubali kusitisha vita katika eneo la Gaza
kwa sababu za kibinaadamu lakini kundi la Hamas limesema kuwa halitakubali tena
makubaliano mengine.
Afisa mwandamizi nchini Israel amesema kuwa makubaliano hayo ya kusitisha
vita yatafanyika kwa saa 24 kufuatia ombi la Umoja wa mataifa.Msemaji wa Hamas ameiambia BBC kwamba uharibifu unao-onekana katika eneo la Gaza wakati wa mchana ndio uliowashinikiza kuendelea na mashambulizi hayo.
Ameishtumu Israel kwa kutumia makubaliano hayo kutekeleza mashambulizi zaidi.
Takriban raia 1000 wa Palestina wameuawa huku zaidi ya raia 40 wa israel wengi wao wakiwa wanajeshi wakifariki.
0 comments:
Post a Comment