Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwembetogwa, Kevin Mlengule
SHULE ya Sekondari ya Mwembetogwa ya Mjini Iringa imepongezwa na wadau wake baada ya hivikaribuni kuwafukuza kazi walimu wanne wa kiume waliobainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike.
“Tunataka shule nyingine ziige mfano wa shule hii, tumefarijika kusikia imechukua uamuzi huo na kwa kufanya hivyo tunaamini shule hiyo itakuwa salama kwa watoto wetu wa kike,” alisema mmoja wa wazazi wenye watoto wanaosoma shuleni hapo, Joachim Mwaikambo.
Mwaikambo alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika shule hiyo ambayo wanafunzi wake “tuliozoea kuwaona wakizurula mitaani wakati wa masomo.”
Naye Jacob Basil aliupongeza uongozi wa shule hiyo akisema; “unadhibiti nidhamu ya wanafunzi na watumishi wake jambo linalotupa faraja wazazi wenye watoto shuleni hapo

0 comments:

Post a Comment

 
Top