kwenda mahakamani ili kupinga mchakato wa Katiba Mpya,
bado uko palepale na kwamba anajipanga.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mchungaji Mtikila
ambaye sasa ni mmoja wa wajumbe walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuunda
Bunge Maalumu la Katiba, alisema amechelewa kutekeleza azma yake kwa sababu ya
kile alichokiita kuwa ni mtego dhidi yake.
Alisema baada ya kuteuliwa kwake, mawakili wake ambao
ni wa nchi za kigeni, walimshauri asitishe kwa muda kufungua kesi hiyo na
kuingia bungeni kwa madai kuwa alichofanyiwa ni mtego kwake.
“Mawakili wangu ambao ni wa nchi za nje wamenishauri kuingia bungeni kwa
sasa kwa sababu kilichofanyika ni mtego kwangu na kinyume chake nitatoa fursa
kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuniwekea pingamizi mahakamani,” alisema
Mchungaji Mtikila.
Alisema hata hivyo azma yake bado iko pale pale na
kwamba atajipanga vizuri ili kuwatetea wananchi katika kudai Tanganyika na
Serikali yao.
Tishio la kiongozi huyo kwenda mahakamani ili kuzuia mchakato wa Katiba,
alilitoa kabla hajateuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba
lililoanza shughuli zake Jumanne, wiki hii.
0 comments:
Post a Comment