Dennis Bergkamp akipozi katika sanamu lake.
SANAMU la mwanasoka aliyeichezea klabu ya Arsenal ya jijini London miaka 11, Dennis Bergkamp limezinduliwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Bergkamp (kulia) akiliangalia sanamu lake wakati wa uzinduzi.
Zoezi hilo lililoshuhudiwa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo limefanyika leo kabla ya mechi ya Arsenal na Sunderland.
Bergkamp ambaye ni raia wa Uholanzi, alijiunga na Arsenal mwaka 1995 na kustaafu kuichezea timu hiyo ya Ligi Kuu England mwaka 2006 baada ya kuiletea mafanikio kadhaa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top