Hizi ni fainali za
20 za kombe la dunia, zijue timu zilizowahi kutwaa ubingwa wa kombe la dunia
pamoja na wafungaji wa michuano hiyo kuanzia mwaka 1930 mpaka
2010.
Mwaka 1930 fainali
ziliandaliwa nchini Uruguay wakati mfungaji bora wa michuano hiyo alikuwa
Muargentina Guillermo Stabile aliefunga magoli nane wakati bingwa wa kombe la
dunia mwaka huo ilikuwa ni timu ya taifa ya Uruguay,.
Fainali za pili za
dunia zilifanyika mwaka 1934 nchini Italy huku Old rich Nejedly akitwaa kiatu
cha dhahabu na Italy walitawaa taji la ubingwa wa dunia.
Fainali za tatu
zilifanyika mwaka 1938 nchini Ufaransa wakati Leonidas wa Brazil alitwaa kiatu
cha ufungaji bora Italy walitetea taji la kombe la
dunia.
Fainali za nne
zilifanyika nchini Brazil mwaka 1950 , mfungaji bora alikuwa mbrazil Admir
aliefunga magoli 8, wakati mabingwa walikuwa ni nchi ya
Uruguay.
Fainali za tano
zilifanyika mwaka 1954 nchini Switzerland mfungaji bora alikuwa Sandor Kocsis
wa Hungary aliefunga magoli 11, kwa mara ya kwanza Ujerumani Magharibi walitwaa
kombe la dunia.
Fainali za sita
zilifanyika mwaka 1958 nchini Sweden, mfungaji bora alikuwa mchezaji wa
kimataifa wa Ufaransa Just Fontaine aliefunga magoli 13, wakati Brazil walikuwa
mabingwa kwa mara ya kwanza.
Fainali za saba
zilifanyika mwaka 1962 nchini Chile, wafungaji bora walikuwa Drazan Jerkovic wa
Czesk, Florian Albert wa Hungary, Garrincha wa Brazil, leonel Sanchez wa Chile,
Valentin Ivanov wa Russia, na Vava wa Brazil wote walifunga magoli manne kila
mmoja, wakatI Brazil walifanikiwa kutwaa taji la dunia kwa mara ya
pili.
Fainali za nane
zilifayika mwaka 1966 nchini England, mfungaji bora alikuwa ni mreno Eusebio
ambaye alifunga magoli 9, huku England kwa mara ya kwanza wakatwaa taji hilo la
dunia.
Fainali za tisa
zilifanyika nchini Mexico mwaka 1970, mfungaji bora alikuwa ni Gerd Muller
alifunga magoli 10, na timu ya taifa ya Brazil ama Selcao walitwaa taji la
dunia.
Fainali za kumi
zilifanyika mwaka 1974 nchini Ujerumani Magharibi, mfungaji bora Grzegorz Lato
wa Poland aliefunga magoli saba, kwa mara ya pili Ujerumani Magharibi walitwaa
kombe la dunia.
Fainali za kumi na
moja zilifanyika nchini Argentina mwaka 1978, Mario Kempes wa Argentina alikuwa
mfungaji bora baada ya kufunga magoli sita, pia Argentina walitwaa taji hilo la
dunia kwa mara ya kwanza.
Fainali za kumi na
mbili zilifanyika mwaka 1982 nchini Hispania , mfungaji bora alikuwa Paulo Rossi
aliefunga magoli sita na na timu ya taifa ya Italy maarufu kama Azuri walitwaa
ubingwa wa dunia kwa mara ya pili.
Fainali za kumi na
tatu zilifanyika mwaka 1986, nchini Mexico, mfungaji bora alikuwa Gary Lineker
wa England baada ya kufunga magoli sita, na Argentina walitwaa ubingwa wa dunia
kwa mara ya pili.
Fainali za kumi na
nne zilifanyika nchini Italy, mwaka 1990, mfungaji bora alikuwa Salvatore
Schillaci wa Italy aliefunga magoli sita, na timu ya Ujerumani Magharibi
wakatwaa ubingwa.
Fainali za kumi na
tano zilifanyika nchini Marekani mwaka 1994, wafungaji bora walikuwa Hrist
Stoichkov, Oleg Salenko wa Russia baada ya kufunga magoli sita, kila mmoja, na
Brazil walifanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia.
Fainali za kumi na
sita zilifanyika nchini Ufaransa mwaka 1998, mfungaji bora alikuwa Davor Suker
alitwaa kiatu cha ufungaji bora, na timu ya taifa ya Ufaransa ilitwaa ubingwa wa
Dunia.
Fainali za kumi na
saba ziliandaliwa na nchi mbili za bara la Asia, kwenye nchi za Korea Kusini na
Japan mfungaji bora alikuwa ni Ronaldo de Lima wa Brazil aliefunga magoli nane,
wakati Brazil walifanikiwa kutwaa taji la dunia kwa mara ya
tano.
Fainali za kumi na
nane ziliandaliwa nchini Ujerumani mwaka 2006, mfungaji bora wa michuano hiyo
alikuwa Miroslav Klose baada ya kufunga magoli matano, huku Italy wakitwaa
ubingwa wa dunia kwa mara ya nne.
Fainali za kumi na
tisa ziliandaliwa nchini Afrika Kusini mwaka 2010, wafungaji bora walikuwa Diego
Forhan wa Uruguay, Thomas Muller wa Ujerumani, Wesley Sneider wa Uholanzi, na
David Villa wa Hispania, bingwa wa alikuwa timu ya taifa ya Hispania maarufu
kama La Roja.
src
shaffihdauda
0 comments:
Post a Comment