Kimelea kinachosababisha Malaria. Mbu hawapendi mazingira ya
baridi.
Watafiti kutoka Uingereza na Marekani wanasema kuwa mabadiliko
ya hali ya hewa huenda yakazua ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa
Malaria kote duniani huku ugonjwa huo ukienea katika maeneo ya milimani barani
Afrika na Amerika ya Kusini.
Katika matokeo ya utafiti yaliyochapishwa kwenye jarida la Science,
wanasayansi hao wanasema hata ongezeko dogo katika viwango vya joto siku za
usoni huenda likaongeza kwa mamilioni maambukizi ya malaria.
Mbu anayesababisha malaria.
Watu wanaoishi katika maeneo ya nyanda za juu wanakosa kinga na hivyo kurahisisha maradhi ya malaria kuenea.
Takriban watu milioni mia mbili ishirini kote duniani huambukizwa ukonjwa wa malaria.
SRC
BBC-SWAHILI
0 comments:
Post a Comment