MSANII wa muziki wa R&B, Bernard Paul ‘Ben Pol’, amewataka wasanii wa Bongo kuwaunga mkono Diamond na AY baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye kampeni ya kilimo inayohamasisha vijana wa Afrika kukipa nafasi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ben Pol alisema kwa jinsi anavyowajua wasanii wa Tanzania, wataanza kuwekeana mtimanyongo bila sababu ya msingi, badala ya kuwapongeza na kuwapa sapoti.
“Ninachoweza kusema ni kwamba, hao ni ndugu zetu na wamekwenda kutuwakilisha vizuri, hakuna haja ya kuwa na hasira nao, kwa sababu wanatuwakilisha wote na hatuwezi kualikwa wote katika kampeni moja, hivyo ni kujitahidi kufanya kazi ambazo zitamvutia mtu kukupa kazi yake,” alisema.
Alisema kwa sasa yupo katika maandalizi ya kusambaza kazi yake mpya, ambayo ana uhakika itafanya vizuri kutokana na ubora wa mashairi yaliyopo ndani yake.
Ben Pol anatamba na nyimbo zake kama ‘Jikubali’, ‘Number One Fun’, ‘Maneno’, ‘Nikikupata’, ‘Samboila’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
0 comments:
Post a Comment