MSANII anayekuja kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini, Maria Joseph ‘Vanessa’ amevunja ndoa yake na kudai talaka baada ya kuchoshwa na tabia isiyoridhisha ya mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Laurence na kuanza maisha ya ubachela.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Vanessa alisema kuwa mume wake huyo alikuwa na tabia ya kubadili wanawake na alikuwa anakuywa pombe kupita kiasi, kitu ambacho kilikuwa kinamnyima raha, ndipo akachukua uamuzi wa kuomba kuachana naye.
“Nilishindwa kuvumilia tabia za uhuni za aliyekuwa mume wangu, kwani alikuwa na kawaida ya kubadili wanawake kila wiki huku akinywa pombe kupita kiasi, ndiyo maana nikaona hakuna haja ya kukaa katika hali ya mashaka, nikadai talaka yangu naye akanipa,” alisema Vanessa.
Msanii huyo wa kundi la sanaa za maigizo la Hamadombe lililopo Kigamboni, alisema kwamba baada ya kuachana na mwanaume huyo, hapendi kuolewa tena, kwani anaona wanaume wote wana tabia kama ya aliyekuwa mumewe na kilichobaki akili yake anaielekeza kwenye uigizaji.
“Akili yangu kwa sasa naielekeza kwenye sanaa, sitaki tena mwanaume, kwani naona wote wana tabia kama ya aliyekuwa mume wangu, hivyo kundi la Hamadombe naliona kama ndiyo mume wangu, kwani ndiyo linanipa pesa ya kujikimu kwenye maisha yangu,” alisema Vanessa

src
TZ daima

0 comments:

Post a Comment

 
Top