Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema baada ya vibaka hao kumpora pochi dada huyo, walitaka kutoweka na bodaboda ndipo wananchi walifanikiwa kumkamata aliyeipora pochi hiyo akaanguka chini wakaanza kumpa kipigo huku mwenzake akifanikiwa kuondoka.
Kama waswahili wasemavyo za mwizi arobaini, kibaka huyo aliyekuwa akiendesha bodaboda kwa kasi, hakufika mbali pikipiki yake ikapata pancha naye akakamatwa na kuanza kupewa kichapo kisha walikusanywa pamoja wakavishwa matairi na kuchomwa moto.
Baada ya kuteketea kwa moto, polisi walifika eneo la tukio wakachukua mabaki ya miili ya vibaka hao na kuipeleka tatika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
(Picha/Habari na Makongoro Oging'/GPL)
0 comments:
Post a Comment