Mwili wa marehemu Asha Mohamed Shiengo 'Mama Tunda' ukiombewa kabla ya mazishi.
Afande Sele akiweka udongo kwenye kaburi la mke wake Mama Tunda leo jioni katika makaburi ya Kolla yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
Afande akiwa na simanzi nzito wakati wa mazishi hayo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania 'TAFF', Simon Mwakifwamba akimpa pole Afande Sele.
Afande Sele akiwa na mwanaye, Asantesana kabla ya mazishi.
Mwanamuziki Profesa Jay (kulia) akimfariji Afande Sele.
MAMIA ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania 'TAFF', Simon Mwakifwamba wameungana kumzika mke wa mwanamuziki Seleman Msindi 'Afande Sele', marehemu Asha Mohammed Shiengo (34) 'Mama Tunda' katika makaburi ya Kolla yaliyopo mkoani humo.
Mama Tunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa Malaria.

0 comments:

Post a Comment

 
Top