STAA wa Sikati Tamaa, Shariff Sadick Ramadhan ‘Darasa’ yupo mbioni kurudi darasani baada ya kufanya muziki muda mrefu.
Akifunguka hivi juzikati katika mahojiano na Kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa na Global TV Online kupitia mtandao wa Global Publishers, Darasa alisema mpango alionao kwa sasa ni kuangalia upande wa pili ambao ni elimu.
“Kila mtu anajua picha ya mtaani jinsi ilivyo, najaribu kujipanga kwenda darasani ili nibalance kwenda sehemu nyingine, pia ni kitu ambacho nimekiweka mbele kuliko kitu kingine chochote na kwenye maisha ya mtaani naishi maisha ya kawaida ambayo mtu akipata anakula na akikosa anakomaa,” alisema.
Darasa amezungumza mengi sana kuhusiana na muziki na maisha yake kwa ujumla
src
GPL
0 comments:
Post a Comment