Roma alia kubanwa kwenye ‘KKK’


MKALI wa muziki wa hip hop nchini, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amevilalamikia baadhi ya vyombo vya habari kwa kukataa kupiga wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la ‘KKK’ hadi atakapofuta baadhi ya mashairi yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Roma alisema kwa kuwa anahitaji wimbo wake upigwe redio zote, amelazimika kufuta baadhi ya vipande hivyo vya mashairi.
“Nashukuru Mungu wimbo wangu umepokewa vizuri na unapigwa sehemu mbalimbali, ingawa kuna changamoto ambazo nimekutana nazo. Lakini najua ndiyo maisha yanavyokwenda, hivyo ni kawaida tu.
“Mimi nyimbo zangu huwa zinaongea ukweli na unayeyafanya hayo ukisikia lazima utapata hasira, kutokana na hilo baadhi ya Ma DJ wakawa wanagoma kuupiga, ndiyo sababu ya kupunguza mashairi ya wimbo huo,” alisema Roma.
Roma ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo, kutokana na ubora wa mashairi ambayo anayatunga na kukubalika katika jamii

src
Tz Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Top