Warren Buffett.
Akiwa na mali yenye thamani ya dola za Marekani Bilioni 62, Warren Buffett ndiye binadamu tajiri kuliko wote duniani. Mwaka 1962 wakati akianza kununua hisa katika kampuni ya Berkshire Hathaway, hisa moja ilikuwa na thamani ya Dola 7.50.Leo, Warren Buffett, akiwa na umri wa miaka 78, ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo na hisa moja hivi sasa ina thamani ya dola 119,000.
Zifuatazo ni baadhi ya njia alizopitia na kuzitumia kuelekea kwenye utajiri alionao, ambazo hata wewe ukizifuata, unaweza kufanikiwa.
• Wekeza faida unayopata:
Unapopata faida katika biashara yako yoyote, mtu huwa anafikiri katika kuitumia. Unashauriwa kutoitumia kwa kuipoteza, bali kuwekeza tena kwenye biashara nyingine au kuongeza mtaji wa kwanza.
Warren Buffett alijifunza hili mapema kabisa. Akiwa shuleni, yeye pamoja na rafiki yake walinunua mashine ya mchezo wa mpira na kuiweka katika saluni ya kunyolea ambayo watu walienda kucheza.
Hela walizopata waliweka na kununua mashine zaidi hadi zikafikia nane.
Katika umri wa miaka 26, alikuwa na kiasi cha dola 174,000, kiasi cha zaidi ya milioni moja kwa sasa. Hata kiasi kidogo cha pesa, kinaweza kugeuzwa na kuwa biashara kubwa.
• Nia ya dhati ya kutaka kuwa tofauti
Siku zote unapaswa kuwa mwenye kuamini zaidi katika mawazo yako badala ya watu wengine. Warren Buffett alipoanza biashara mwaka 1956, aliwakusanya wenzake na kuanza mtaji wakiwa na dola 100,000 na wakanunua hisa. Wengi walijua atafeli, lakini miaka 14 baadaye hisa zao zilikuwa na thamani ya dola milioni 100.
Badala ya kufuata mawazo na biashara zilizozoeleka, yeye aliamua kuwafuata makapuku wenzake na kufanya uwezekaji unaomwingizia hela nyingi kila mwaka.
• Jiamini katika kutoa maamuzi
Watu wengi hushindwa kuyafikia mafanikio kwa sababu ya kutojiamini wakati wa kutoa maamuzi yanayohusiana na biashara wanazozifanya.
Siyo vibaya kukusanya maoni ya marafiki au ndugu, lakini mwisho wa siku uamuzi ni lazima uwe wa kwako. Warren Buffett anajivunia kuwa mwenye maamuzi ya busara na anayefanyia kazi mawazo yake.
Wakati watu wanapomtafuta kwa ajili ya biashara, huwaambia kwamba kitu cha kwanza kabisa kufungua mazungumzo yao ni lazima iwe bei.
• Ifahamu biashara kabla hujaanza
Unashauriwa kila mara kufanya mapatano ya biashara yoyote kabla hujaianza. Ni lazima ujue kazi utakayoifanya na malipo yatakayotolewa na kila upande uridhie. Warren Buffett alijifunza elimu hii akiwa mdogo, pale bibi yake alipompa kazi ya kulima bustani ya familia yeye na rafiki yake.
Waliifanya kazi hiyo kwa muda wa saa tano, lakini wakati wa malipo, bibi yao aliwalipa senti tisini ambayo nayo walitakiwa kugawana. Akajutia nguvu zake zote alizotumia kwa masaa mengi akilinganisha na malipo. Kila mara jitahidi kujua utakavyofaidika kwa unachoenda kukifanya, hata kama unafanya biashara na ndugu au marafiki.
• Fuatilia matumizi madogomadogo
Warren Buffett aliwekeza katika biashara zilizokuwa zikiendeshwa na mameneja ambao kazi yao kubwa ni kuangalia matumizi. Hii ilitokea baada ya kumshuhudia mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza karatasi za chooni akihesabu toilet paper mojamoja ili kuona kama ni kweli kwenye boksi kulikuwa na vipande 500. Na kweli akakuta amedanganywa.
Na tena kuna siku alimpa kazi ya kupaka rangi na kumlipa rafiki yake, lakini baadaye akaja kubaini kuwa jengo lake lilipakwa upande mmoja tu, ule unaongalia barabarani. Unashauriwa kufuatilia kwa karibu kila gharama unazotumia maana unaweza kukuta kuna upungufu.
src
GPL
0 comments:
Post a Comment