WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba wanaendelea na mchakato wa kupitia vifungu vya Rasimu katika ngazi ya kamati, kabla ya keshokutwa kuanza rasmi mjadala wa namna gani Tanzania inaweza kupata katiba mpya, miaka 50 baada ya kuungana kwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Katika hatua za awali ngazi ya kamati, tumeshuhudia mambo mengi hasa yanayohusu hatima ya Muungano, ambao umekuwa ndiyo simulizi kuu katika mchakato mzima.
Kwa miaka mingi Watanzania tumeishi tukiaminishwa kuwa Muungano huu uko safi na yeyote aliyeonekana kuuzungumzia kwa namna ya kuukosoa, alichukuliwa kama msaliti, mhaini na mtu asiye na nia njema na nchi yetu.
Mambo mengi yanayohusu uhusiano wa nchi hizi mbili umekuwa siri kubwa, baadhi ya mambo yameharibika au kwenda mrama kwa kuwa kila mmoja alikuwa hataki kuonekana kama ndiye chanzo cha kuyumba au kuvunjika kwake.
Yanayotokea hivi sasa mjini Dodoma ndiyo kielelezo cha ninayosema, kwa sababu sasa watu wameanza kuhoji ilipo hati ya Muungano na uhalali wake. Kitu hiki, japo ni fahari ya taifa, lakini kimefanywa kuwa siri na mtu anayeulizia anaonekana kama vile siyo mwenzetu.
Wapo baadhi ya wanasiasa, hasa kutoka Chama Cha Mapinduzi wanaogopa kuuzungumzia Muungano kwa ukweli wake, wanadhani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na waasisi wake, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Hawataki tujadili matatizo yake, wanataka tujifanye kama vile hatuoni, tuendelee tu kuwapuuza watu wanaoukosoa, hata kama watakuwa na hoja zao zenye mashiko.
Ni bahati mbaya kwamba CCM haitambui kuwa hakuna Mtanzania mwenye kutaka kuona Muungano huu ukivunjika. Kila mmoja anataka uendelee kuwepo. Tofauti pekee ambayo watu wanayo, ni juu ya namna gani muundo wake uwe.
Njia pekee ya kupata namna nzuri ya aina ya Muungano tunaoutaka, ni kuwaruhusu watu, bila kujali wana itikadi gani za kisiasa, wauchokonoe, waupinduepindue miguu juu kichwa chini, waupekeche na kujua kila kizuri na kibaya kilichomo ndani yake.
Ni hapo ndipo tutakapojua wapi tulikosea, wapi hatukupitia na vipi turekebishe ili twende sawa. Muungano wetu una kasoro na mojawapo ni hadhi bandia ya nchi ya Zanzibar. Ingawa katiba yake, ambayo pia inaikiuka ile ya Muungano, inaitaja kama nchi yenye mamlaka yake kamili, lakini ukweli wa mambo hauko hivyo.
Haya ni mambo yanayopaswa kuzungumzwa kwa uwazi na bila kutegeana. Kama inatambuliwa kama nchi, basi na Bara nayo lazima iwe nchi. Tukizungumza namna hii, tutaelewana tu badala ya kutengeneza mazingira yanayolazimisha utashi wa upande mmoja.
Muungano wetu umekuwa ni wa kuungaunga ili kukidhi mahitaji ya nyakati bila kuangalia athari zake kwa upana. Tulikubali Zanzibar irekebishe katiba yake ili kupooza moto uliokuwa unaonekana kuwaka baina ya vyama viwili vikubwa vya CCM na CUF, bila kujiuliza ni vipi watu wa Bara nao wakitaka usawa wa aina hiyo.
Kama tutaijadili rasimu hii vizuri na kwa nia njema, ni lazima Katiba ya Zanzibar nayo itaguswa, ambayo huenda na yenyewe ikalazimika kufanyiwa marekebisho. Jambo moja la msingi ni kwamba mchakato huu tuufanye kwa nia ya kupata katiba bora na siyo bora katiba.
Tunaweza kujidanganya kwamba tutafanya mbinu hii na ile ili kupitisha katiba isiyojibu maswali mengi ya msingi, lakini lazima tujue kuwa tunapoteza tu muda kwa sababu wakati wa mabadiliko hauepukiki.
Watu lazima wawe tayari kupoteza baadhi ya vitu kwa masilahi ya wengi. Na ni lazima tupate muda wa kutosha wa kujadiliana, kifungu kwa kifungu, mstari kwa mstari. Tusifanye haraka ili tuwahi, kama kuna kitu ni lazima kifanyike sasa badala ya mjadala wa katiba, basi tuahirishe hili la muhimu, tulipishe hilo la muda huu.
Wiki mbili zilizopita tumekuwa tukichambua ugonjwa wa kansa ya titi katika safu hii, leo tunaeleza dalili za maradhi haya.
Najua wanawake wengi wanajiuliza ni zipi dalili za saratani ya matiti?  Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi.
Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti. Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza au ambao hauko thabiti, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yoyote.
Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi. Dalili nyingine ni pamoja na  kuwepo uvimbe kwenye sehemu za kwapa, sehemu ya titi kuingia ndani, hali inayoashiria uvimbe usioonekana au usioweza kuhisiwa na mabadiliko kwenye chuchu, kama vile chuchu kuzama ndani au kuwa na nundu ndogondogo, chuchu kuwasha, kuhisi kama kuchoma, kidonda kwenye chuchu au chuchu kuwa na kovu ambalo huashiria saratani ya sehemu hiyo.
Dalili nyingine za kansa ya matiti ni kubadilika kwa umbo la titi na rangi ya ngozi kuwa nyekundu (redness/rush), ngozi ya titi kuwa kama ganda la chungwa (skin changes)  na kuongezeka kwa joto kwenye titi. Dalili hizi huashiria kusambaa kwa saratani mwilini.
Dalili nyingine ni chuchu kutoa maji ambayo hayana rangi. Mara nyingine chuchu hutoa majimaji yenye rangi tofauti.
Baada ya kuzijua dalili kwa kawaida mgonjwa hushauriwa kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na wataalamu wa afya ili kuweza kutambua kuwepo tatizo hili na baada ya hapo kufanyiwa vipimo vifuatavyo ili kusaidia kutambua ugonjwa huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Top