Na Faustine Ruta, Bukoba — Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Dk Ian McClements aliwasili Bukoba asubuhi ya Jumatatu, Mei 5, 2014 kwa ndege ya kukodi.
McClements akiwa Bukoba alikagua uwanja wa Kaitaba, na baadaye akakwea tena ndege yake kuelekea jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Dk. Ian McClements akiteta jambo na Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA kwenye Uwanja wa Kaitaba, Jumatatu Mei 5, 2014.
Viwanja hivi vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
Dk. Ian McClements (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Nje kidogo ya mipaka ya uwanja Dk. Ian McClements analazimika kuchimba ili aweze kuona chini kuna nini? Akitaka kupima maji yanafyonzwa vipi na ni udongo gani? Je, maji yananyonywa vipi na udongo wa hapa Kaitaba, kwenye uwanja huu huu wanaotaka kuuwekea nyasi za bandia?
Kumbe kuna mchanga chini, safi.
Dk. Ian McClements akichimba chini ili kupima na kuona udogo upi ulipo chini, Amehimba katika maeneo matatu tofauti tofauti na kubaini tofauti.
Dk. Ian McClements (kulia) akichukua kumbukumbu kushoto ni Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba.
Dk. Ian McClement akipima kina
Dk. Ian McClement alimwaga maji ndani ya shimo ili kuona kaji nini kitafata na je yatanyonywa na udongo kwa muda gani!
Ilichukua muda wa dakika 1 na sekunde 40 na maji yalikuwa yameshatoweka
Akipima maji aliyoweka
Dk. Ian McClements akichukua maelezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Alichimba na sehemu ya upande wa pili wa goli
Hapa mchanga hakuna na udongo wake ni mweusi mchanga upo chini zaidi
Dk. Ian McClements baada ya kumaliza kazi yake alipaa kuelekea jijini Mwanza na hapa alikuwa anaagana na Jumanne Chama kwenye Uwanja wa Ndege
0 comments:
Post a Comment