Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa utandawazi na hasa mitandao ya kijamii inawaharibu watanzania na hata vijana,sijui tatizo nini hapa au uwelewa wetu mdogo,watu wanatengeneza mamilio kwa kutumia mitandao hiyo ya kijamii,watu wengi wanapata taarifa kwa haraka kupitia mitandao,tunapata taarifa mbalimbali za kuwasaidia watanzania kupitia mitandao,Imeongeza uelewa mkubwa kwa kundi ambalo lipo tayari kujifunza.Kama tungetumia fursa hii vizuri utandawazi ungetunufaisha,kwa mfano kama serikali ingeamua kutumia fursa hii ya mitandao mfano kuweka materials mitandaoni wanafunzi wakasoma, kingeanzishwa kitengo cha elimu mtandaoni ambapo maada mbalimbali zingekuwa zinawekwa huko facebook,wanafunzi wangesoma,kama wanapenda facebook wafate hukohuko,badala ya kualumu kuwa mitandao inawaharibu wnafunzi hii ni kwa sababu tumeacha watu waweke uchafu tu.Hii ni soko huria, shule hazina vitabu lakini hatutumii fursa ya kuweka soft copy ili wanafunzi wasome,tungefungua page ambazo zingewekwa materials ili wanafunzi wasome.
Badala yake tumeacha mitandao hii iwe sehemu ya watu kujinadi maungo yao,kutafuta wanaume,kutukanana.kuchafuana,na kuweka picha za utupu.
Sheria lazima ziende na wakati,kwa mfano unafungia wimbo kisa haukidhi maadili ya kitanzania lakini wimbo ushawekwa you tube na kuangaliwa mara nyingi ukienda kwenye vibanda vya kuingizia nyimbo unapata na kuweka kwenye simu yako.Badala ya kufungia ni bora wakatozwa faini ili wasirudie,unafungia wimbo wakati club unapigwa na msanii anaimba kwenye matamasha ifike wakati tukubaliane dunia inabdilika,watu wanabalehe mapema sana na hii ni soko huria tuache watu wajue lipi zuri lipi baya.


Bila weredi wengi tutapotezwa na mitandao ya kijamii lakini kiuhalisia mitandao ni sehemu ya kutengeneza hela ya maana.Mjinga asipojua kuwa yeye ni mjinga ni shida.Mpumbavu siku zote atakuwa mtaji wa wenye akili tumia fursa ya mitandao tengeneza hela!
0 comments:
Post a Comment