
MSICHANA Zuhuru Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar, ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75 na kumsababishia maumivu makali, anahitaji kiasi cha shilingi 5,000,000 ili aweze kufanyiwa upasuaji nchini India.
Daktari huyo ambaye pia alimtibia mtoto Hamisi aliyekuwa na matatizo kama hayo ambaye hali yake inaendelea vyema, alisema msichana huyo atarejea katika hali yake ya kawaida endapo ataweza kufika hospitalini kwake na kumpangia kwa ajili ya upasuaji hapo Oktoba 25, mwaka huu.
Zuhura amewaomba Watanzania kumsaidie ili kuweza kupata matatibu hayo aweze kupona na kuendelea kuwalea watoto wake ambao ni wadogo wanaohitaji msaada wake kama mama na kwamba aliyeguswa na tatizo linalomkabili anaweza kumsaidia kupitia simu yake ya mkononi namba 0717319555.
0 comments:
Post a Comment