Kitaalamu, tatizo hilo hujulikana kama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana
Tatizo la kuota matiti kwa
wanaume na watoto wa kiume limekuwa kubwa katika dunia ya leo.
Inawezekana wakati unatembea
njiani ukaona wanaume au watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti tena
makubwa ambapo watu wengi huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu,
tatizo hilo hujulikana kama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu
ya kwenye titi inayojulikana kama glandular tissue.
Tatizo hili huonekana zaidi kwa
watoto wachanga na wanaume walio katika umri wa kubalehe, lakini pia
huonekana kwa watu wazima na wazee.
Ukubwa wa tatizo
Asilimia 60-90 ya watoto wachanga
wanapata tatizo hili la kukua kwa matiti kwa mpito linalojulikana kitaalamu
kama, transient gynecomastia kutokana na kuwepo kwa kichocheo cha aina ya
estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wa mama.
Kati ya asilimia 4-69 ya vijana
walio katika umri wa kubalehe imeonekana wanapata tatizo hili kutokana
na kuwepo kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya estradiol. Mara nyingi
huonekana katika umri kati ya miaka 10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi
18, si kawaida yake kuonekana kwa vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 17.
Asilimia 24-65 ya watu wazima
hupatwa na tatizo hili, hii hutokana na kubadilishwa kwa wingi kwa
kichocheo aina ya testosterone kuwa estradiol na kutolewa kwa uchache kwa
kichocheo hiki cha testosteron kutoka kwenye korodani ziazoanza
kuzeeka..Ikumbukwe ya kwamba kichocheo hiki testosteron hutengenezwa katika
korodani. Kichochezi cha testosteron ndicho kichochezi kikuu cha kiume
kinachowezesha tabia za kimwili za kiume.
Nini hutokea?
Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa
wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kitaalamu
kama, estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa
wingi ama kuongezeka kwa msisimko wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya kawaida
kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu.
Kichocheo hiki husababisha
chembechembe zinazojulikana kama ductal epithelia kuongezeka kwa wingi,
kurefuka na kugawanyika, kuongezeka kwa chembechembe za mafuta na kuongezeka
kwa mfumo wa damu kwenye matiti hutengenezwa kutoka kwenye vichocheo vya
testosteron na androgen kwa kutumia kimeng’enyo kinachojulikana kama aromatase.
Aina za tatizo hili
-Puffy nipples –Kuongezeka ukubwa wa chuchu za matiti
kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular
Pure glandular gynecomastia –
Huonekana zaidi kwa wale wanaofanya mazoezi ya kujenga mwili, kutokana na
matumizi ya dawa za kujenga mwili ambazo zinakuwa na kiwango kikubwa cha
kichocheo aina ya testerone, ambacho hubadilishwa kuwa estrogen.
Kwa wanaume wembamba, tatizo hili
hutokea kutokana na kuongezeka kwa tishu za tezi za maziwa (breast tissue
gland) pamoja na kuwepo/kutokuwepo kwa tishu aina ya adipose.
Ni nani aliyeko hatarini?
-Wanaume walio na umri zaidi ya
miaka 50.
-Wenye uzito uliopitiliza
-Unywaji pombe kupindukia
-Magonjwa sugu ya figo au ya ini
-Kuwepo kwa historia ya tatizo
hili katika familia.
Visababishi vya kukua kwa matiti
kwa wanaume
-Pseudogynecomastia – Kuongezeka
kwa tishu zinazozunguka chuchu za matiti na huambatana na kuwepo kwa wingi wa
tishu aina ya adipose. Mazoezi na kula vyakula venye virutubisho sahihi
huondosha tatizo hili.
-Unilateral/asymetrical
gynecomastia – Ni kuongezeka kwa titi moja pekee au la upande mmoja wa mwili wa
mwanamume kutokana na sababu mbalimbali. Titi la upande wa pili huwa kwenye
umbile na saizi ya kawaida. Bilateral gynecomastia ni kuongezeka
kwa matiti yote mawili.
-Hypogonadism – Kutofanya kazi
kwa korodani vizuri na kuwa ndogo. Hii husababishwa na magonjwa
mbalimbali. Umri – Kuzeeka pia kumehusishwa kutokea kwa tatizo
hili kutokana na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo cha testerone
na kuongezeka kwa juhudi za kutengeneza kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya
estradiol kutoka kwenye kichocheo aina ya testerone.
Pia, mabadiliko ya mfumo mzima wa
vichocheo mwilini hasa kwa wale wenye uzito uliopitiliza.
-Uzito uliopitiliza – Watu wenye
uzito uliopitiliza hupatwa na tatizo hili kutokana na kuharibika kwa mfumo wa
vichocheo mwilini na hivyo kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen mwilini
mwao na wakati huohuo kupungua kwa kichocheo kingine aina ya testerone.
-Saratani – Baadhi ya saratani
kama vile ya kwenye korodani, tezi lililo juu ya figo, saratani ya tezi la
kichwa, huharibu mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa wa kuweka sawa vichocheo
kati ya uanaume na uanawake (male-female hormonal balance).
-Hyperthyroidism – Kukua kwa ukubwa wa tezi la koo na
hivyo kutengeneza kwa wingi
kichocheo aina ya thyroxine.
- Tatizo la figo kushindwa
kufanya kazi - Nusu ya wagonjwa wote wanaotibiwa tatizo la figo kushindwa
kufanya kazi kwa kutumia hemodialysis hupatwa na tatizo hili la kukuwa kwa
matiti kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini.
-Matatizo ya Ini – Dawa za
kutibu magonjwa ya kwenye Ini kama kuoza kwa ini, ini kushindwa kufanya
kazi husababisha kutokea kwa tatizo hili kutokana na kukosekana kwa uwiano sawa
wa mfumo wa vichocheo mwilini.
-Utapiamlo, ukame – Utapiamlo,
ukame au kujikondesha husababisha kupungua kwa kichocheo aina ya testerone na
kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen na hivyo kuharibu mfumo wa vichocheo
mwilini.
Hii hutokana na kukosekana kwa
virutubisho sahihi mwilini ambavyo vingi husaidia kurekebisha mfumo wa
vichocheo mwilini na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa mbalimbali pamoja
na tatizo hili.
-Madhara ya dawa za kurefusha
maisha (ARVs) kwa wagonjwa wa Ukimwi.
-Utumiaji wa dawa za kulevya kama
bangi/marijuana.
Src
mwananchi
0 comments:
Post a Comment