- Bunge la Katiba ni mfano mmoja tu
WIKI hizi nafarijika kwamba baadhi ya mambo niliyoyaandika huko nyuma katika safu hii na kupingwa vikali katika mitandao, sasa ukweli wake unadhihirishwa na tafiti za kisayansi zinazofanyika nchini.
Wiki iliyopita nilifarijika tena baada ya kusoma utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza uliohusisha Watanzania 1,425 wa sehemu mbalimbali nchini. Utafiti huo uliibuka na matokeo ya kushtua na kushangaza kuhusu sisi Watanzania tulivyo – yaani hulka zetu.
Kwa mfano, pamoja na ufisadi wa IPTL kuandikwa na kutangazwa sana na vyombo vya habari vya hapa nchini kwa karibu miaka 10, bado zaidi ya asilimia 78 ya watu waliohojiwa wamesema hawana habari nao – yaani hawafahamu lolote kuhusu jambo hilo. Vivyo hivyo kwa ufisadi mwingine kama ule wa EPA, Richmond, ununuzi wa rada nk.
Hebu fikiria: Zaidi ya Sh. bilioni 123 zilichotwa na mafisadi katika skandali hiyo ya EPA lakini asilimia kubwa ya Watanzania hawajui lolote kuhusu ufisadi huo licha ya kuandikwa sana na vyombo vya habari!
Hivi Watanzania hawa wanawezaje kuchukua hatua kuiwajibisha serikali kwa kukumbatia ufisadi kama hata masuala yenyewe hawayafuatilii? Hivi Watanzania hawa wanawezaje kujitokeza siku ya uchaguzi kupiga kura na kuchagua viongozi bora kama hata hawajali masuala kama hayo?
Hii inanifanya nikubaliane kabisa na msomaji wangu mmoja ambaye alisema Watanzania tuna tatizo la ujinga wa kijumla - collosal mass ignorance.
Nina hakika ni ujinga huo wa kijumla unaowafanya Watanzania wengi (hususan vijana) wasijali sana kinachoendelea katika Bunge la Katiba licha ya kwamba mapesa mengi ya walipakodi yanateketezwa na bunge hilo.
Vijana ndiyo hovyo kabisa. Kutwa nzima – wakiwa kazini, kwenye mabaa au katika vigenge vyao hujadiliana masuala yasiyo ya msingi kama vile muziki wa bongo fleva au ligi kuu ya soka ya England, na si kuteketezwa kwa pesa zao (za umma) na Bunge hilo la Katiba.
Hawana muda na suala la Katiba mpya licha ya kwamba mustakabali na ustawi wa maisha yao binafsi utategemea sana huko mbeleni na vifungu vya Katiba vitakayoamuliwa na Bunge hilo.
Hulka hii ya ujinga wa Watanzania, ambayo sasa imethibitishwa tena na utafiti huo wa Twaweza, ndiyo iliyonichochea kuandika makala ile ya Mei 2014, kwenye safu hii, iliyozungumzia matokeo ya utafiti mwingine wa kimataifa ulioonyesha ya kuwa Tanzania tunashikilia nafasi ya tisa duniani katika orodha ya nchi zenye wananchi wenye uwezo mdogo wa kufikiri!
Makala hiyo iliibua mjadala mkubwa mitandaoni huku wengine wakinilaumu kwa kuamini utafiti huo ‘uliofanywa na Wazungu’. Nakumbuka hata Naibu Spika, Mh. Ndugai alikejeli suala hilo wakati lilipoibuliwa bungeni na mbunge mmoja wa Upinzani.
Akimjibu mbunge huyo (simkumbuki jina) Mh. Ndugai alisema kuwa si kweli kwamba Tanzania tunashika nafasi ya tisa duniani kwa uwezo mdogo wa kufikiri, na akamlaumu mbunge huyo kwa ‘kuokoteza’ taarifa za mitandaoni.
Sasa, baada ya utafiti huo wa Twaweza kuibuka na matokeo hayo ya jinsi Watanzania wasivyojali masuala muhimu yanayogusa maisha yao kwa njia hasi, kina Ndugai wataendeleaje kukataa kwamba Watanzania tunaongoza kwa kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri? Wataendeleaje kupuuza matokeo ya utafiti huo kwa madai kuwa ni “taarifa za kuokoteza mitandaoni”?
Ndugu zangu, nirudie nilichopata kusisitiza huko nyuma: Kama mambo yanakwenda shagalabagala hapa Tanzania (kwa mfano Bunge la Katiba), si kwa sababu ya werevu wa chama tawala CCM au wa serikali yake; bali ni kwa sababu ya ujinga wetu Watanzania!
Baada ya matokeo ya utafiti huo wa Twaweza, sasa naamini pasi shaka yoyote ya kwamba ni kweli Tanzania tunashika nafasi ya tisa duniani katika orodha ya mataifa yenye wananchi wenye bongo zenye viwango vya chini vya kufikiri – wenyewe huita IQ - yaani Intelligence Quotient.
Kwa faida ya wale ambao hawakuisoma makala yangu hiyo ya Mei 2014, nirudie kueleza tena kwamba IQ hupimwa kwa kuangalia uwezo wa ubongo wa kupembua aina mbalimbali za taarifa, na kwamba katika orodha ya The Top 10 Countries With the Lowest Population IQ sisi Tanzania tunashika nafasi ya tisa.
Tunashika nafasi ya tisa tukiwa na wastani wa kiwango cha IQ 72. Nafasi ya 10 inashikiliwa na Sudan ambayo pia kiwango chake ni 72.
Kwa mujibu wa orodha hiyo, Ghana inashika nafasi ya 8 kwa wananchi wake kuwa na kiwango cha chini cha IQ yaani 71.
Nafasi ya saba ni Nigeria (67), nafasi ya sita ni Guinea (66), nafasi ya tano ni Zimbabwe (66), nafasi ya nne ni DR Congo (65), nafasi ya tatu ni Sierra Leone (64), nafasi ya pili ni Ethiopia (63) na nafasi ya kwanza ni Equatorial Guinea (59).
Sasa, unatarajia nini kutoka kwa nchi (Tanzania) ambayo inashika nafasi ya tisa kwa uwezo mdogo wa kufikiri? Nchi ya namna hiyo, bila shaka, raia wake hawaji juu wakati maoni yao ya aina ya Katiba mpya wanayoitaka yanapowekwa pembeni kwa matakwa ya chama tawala na serikali iliyoko madarakani.
Nchi ya namna hiyo inayoongoza kwa wananchi wake kuwa na IQ ndogo, bila shaka, wanasiasa wake wa chama tawala na wa Upinzani watakuwa wanazozana wenyewe katika uandikaji wa Katiba mpya huku kila upande ukiweka mbele maslahi ya kichama kuliko ya taifa lao.
Nchi ya namna hiyo, bila shaka, Bunge lake la Katiba likikwama (kama lilivyokwama Dodoma) Rais wake (kama ilivyo kwa Kikwete) atakwenda Texas, Marekani kutembelea maktaba binafsi ya Rais wa zamani wa taifa hilo, George W. Bush, na wananchi wake wataona ni jambo la kawaida tu!
Hiyo ndiyo Tanzania yetu. Tanzania yenye wananchi wenye IQ ndogo. Asante asasi ya Twaweza kwa kufanya utafiti na kuthibitisha, kwa mara nyingine tena, kwamba Tanzania tuna tatizo la collosal mass ignorance. Sijui kama sekondari zetu hizi za kata zitatuondoa kwenye tatizo hilo!
Tafakari

0 comments:
Post a Comment