Oscar alianza msimu
huu akiwa kwenye form nzuri, kiungo mchezeshaji huyo wa kibrazil alifunga mabao
5 katika mechi zake 12 za kwanza premier league na akawa chaguo la kwanza la
Jose Mourinho. Mourinho alijenga kikosi chake kumzunguka Oscar, huku Oscar
akicheza kama namba 10 anayekaba kuanzia juu, akitafuta kufunga au kutoa
assists. Lakini katika miezi ya karibuni kiwango cha Oscar kinaonekana
kupungua.
Kushuka
kiwango
Pamoja na kufunga
mabao 5 katika michezo 12 ya kwanza ya msimu wa EPL, Oscar ameweza kufunga bao 1
tu katika michezo 14 iliyofuatia na huku kiwango chake katika eneo la
kushambulia kikiwa chini. Takwimu zinaonyesha kupiga mipira iliyolenga goli
kumeshuka kwa 44%. Mchoro wa hapo unaonyesha takwimu za mchezo wake jinsi
zilivyoshuka.
Kama tunavyoona
uwezo wake wa kufunga ulivyoshuka kwa kiasi kikubwa. Kutisha kwake kwenye
kushambulia kumepungua na amekuwa hatengenezi nafasi nyingi za kufunga pia,
amejaribu kutengeneza nafasi 36 katika michezo 26. Willian ambaye amecheza mechi
18 pekee ametengeneza nafasi 39, wakati Eden Hazard ametengeneza nafasi
77.
Kwa mchezaji
anayecheza kwenye nafasi yake tulitegemea makubwa zaidi, hata kama Oscar
anafanya kazi kubwa bila na mpira katika pressing.
Oscar hata hivyo
anafanya kazi, katika kukaba na kupora mipira. Lakini, Oscar alishindwa kufanya
tackling hata moja dhidi ya Fulham na taratibu amekuwa akishindwa kulifanyia
kazi hili zoezi, ingawa mpaka sasa ameweza kufanikiwa kwa 59% ya tackling zote
alizojaribu.
Nini
tatizo?
Tatizo hili lilianza
pale Mourinho alipowaelekeza vijana wake kucheza kwa kukaba zaidi, Hii ilikuja
baada ya michezo kadhaa ambayo Chelsea walikuwa wakiruhusu magoli mengi na kisha
wakapoteza mechi ya Capital One waliyotolewa na Sunderland. Tangu wakati huo
Chelsea wamekuwa wakicheza kwa kukaba zaidi huku watatu wa kushambulia
wakilazimika kurudi kukaba zaidi..
Oscar amekuwa
akicheza no. 10, Willian kulia pembeni na Hazard kushoto pembeni, wakati
kumekuwepo na mabadilishano, Oscar amekuwa akirudi kucheza chinizaidi na hivyo
kupelekea mchango wake katika kushambulia uwe mdogo. Dhidi ya Fulham alikuwa
akicheza zaidi katika kiungo cha juu, na sio katika eneo ambalo no. 10
hucheza
Oscar alicheza chini
sana kuliko kawaida. Katika mchezo huu hakufanikiwa kufanya tackling hata moja,
na alijaribu mara tano kufanya hivyo, kitu ambacho hakiridhishi. Huu ulikuwa
mchezo mgumu kwa Oscar, alitengeneza nafasi moja tu. Mwishowe alitolewa kwenye
dakika 77.
Tatizo jingine ni
uchovu. Oscar ni mchezaji ambaye hufanya kazi sana na mfumo wa Chelsea
unamlazimu kucheza kwa namna hiyo. Akirudi nyuma kukaba pamoja kunyang'anya
mipira jambo ambalo linamchosha mno kijana huyo mwenye miaka 22. Oscar
ameshacheza mechi nyingi sana katika misimu miwili ndani ya Chelsea, mpaka sasa
tayari ameshacheza mechi 101, hapo bila kutaja namba ya michezo ya kimataifa
anayoichezea Brazil tangu ajiunge na Chelsea. Ndio maana haishangazi kuona akiwa
amechoka na Mourinho labda hajampumzisha vya kutosha, hivyo Mourinho anahitaji
kumpa mapumziko kiasi ili aweze kupata matunda mazuri kutoka kwa mchezaji huyo
kwa mara nyingine tena.
Hitimisho
Ni vizuri kutambua kwamba Oscar ana umri wa miaka 22 na ataendelea kukua kuimarika kuwa na kiwango kizuri. Amefunga mabao 6 msimu huu, hata kama hivi sasa anakabiriwa na ukame wa mabao. Msimu uliopita aliweza kufunga mabao manne tu kwenye ligi hivyo unaweza kuona amefanya vizuri kuliko msimu uliopita kwenye kufunga. Mfumo wa Mourinho katika kukaba zaidi unamaanisha Oscar anafanya kazi nyingi zaidi kuliko msimu uliopita, jambo ambalo linamkaba mwenyewe katika kufanya vizuri kwenye kushambulia. Anachohitaji sasa ni kufanyiwa rotation na Mourinho na hapo ndipo tutamuona yule Oscar tuliyemzoea.
Ni vizuri kutambua kwamba Oscar ana umri wa miaka 22 na ataendelea kukua kuimarika kuwa na kiwango kizuri. Amefunga mabao 6 msimu huu, hata kama hivi sasa anakabiriwa na ukame wa mabao. Msimu uliopita aliweza kufunga mabao manne tu kwenye ligi hivyo unaweza kuona amefanya vizuri kuliko msimu uliopita kwenye kufunga. Mfumo wa Mourinho katika kukaba zaidi unamaanisha Oscar anafanya kazi nyingi zaidi kuliko msimu uliopita, jambo ambalo linamkaba mwenyewe katika kufanya vizuri kwenye kushambulia. Anachohitaji sasa ni kufanyiwa rotation na Mourinho na hapo ndipo tutamuona yule Oscar tuliyemzoea.
src
shaffihdauda
0 comments:
Post a Comment