Wakati zikiwa zimebakia takribani siku tano kabla ya
wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya kombe la CAF Champions League -
Dar Young Africans kuwavaa mabingwa watetezi Al Ahly katika dimba la Cairo
Stadium uliopo ndani ya mji mkuu wa Misri, Cairo, mtandao huu utakuwa unakuletea
namna gani klabu ya Simba - mahasimu wa Yanga walivyoweza kuvunja rekodi na
kuivua ubingwa Zamalek.
Simba walishinda 1-0 katika mchezo wa kwanza
uliopigwa jijini Dar es Salaam, Yanga nao pia wameshinda 1-0 dhidi ya wapinzania
wao. Kinadharia inaonekana Yanga wana nafasi ya kuvuka kwenda hatua ya mbele kwa
sababu tayari wameshapata ushindi nyumbani, ingawa rekodi yao katika viwanja vya
timu za kiarabu sio nzuri. Ila pamoja na haya Yanga bado wanaweza kuiondoa
kwenye michuano Al Ahly. Simba waliweza hata pia Yanga inaweza, ila kwa mbinu
gani. Swali ni kwa namna gani wataweza kupata matokeo chanya jumapili ijayo
dhidi ya Al Ahly.
Mtandao huu unakuletea mahojiano na katibu mkuu wa
zamani wa Simba Kassim Dewji, akielezea namna ambavyo Simba na watanzania kwa
umoja wao walivyoiwezesha klabu hiyo ya msimbazi kuvunja rekodi na kuitoa
Zamalek ndani ya ardhi yao.
"Kwa kawaida kwa wakati huo ndege inapotoka Dar
hupitia Nairobi kisha Khartoum then Cairo. Kwenye ndege tulikuwa viongozi,
wachezaji pamoja na wazee wa kamati ya ufundi. Mzee mmoja wa kamati ya ufundi
alituambia lazima ili vitu vikae sawa lazima tufike Cairo kwenye muda
aliotupangia, sisi kama viongozi tulishajua kwamba suala lile halitowezekana kwa
sababu ndege lazima ingepita Khartoum - Sudan kwanza hivyo tusingefika Cairo
muda aliotaka, tulipomwambia hivyo akasema tumuachie yeye atajua cha kufanya na
tungefika Cairo muda uliotakiwa.
"Tulipokuwa tunakaribia Khartoum, pilot alipokuwa
akifanya mawasiliano na wenzake uwanja wa ndege wa Khartoum akaambiwa hali ya
hewa ni mbaya sana, mpaka tunafika Khartoum pilot alishindwa kuuona hata uwanja
wenyewe na hivyo ikamlazimu kupeleka ndege moja kwa moja mpaka Cairo na tukafika
muda ule ule aliotaka yule mtaalam."
"Tangu tunafika kule wote tulikuwa tunajua hila
na karaha za wapinzani wetu hivyo tulijidhatiti kukabiliana na hali yoyote ya
kutoodhofisha. Uwanja ndege tuliposhuka kwa sababu kuna wenzetu walikuwa
wameshatangulia hivyo walikagua basi tuliondaliwa na kulisafisha kwa kila namna
kuhakikisha lilikuwa na usalama. Tuliondoka na kuelekea kwenye hoteli
waliyotuandalia.
HOTELINI - CHAKULA
"Tulipofika hotelini tukavifanyia uchunguzi
vyumba vyote, tukaridhika tukawaruhusu wachezaji waingie vyumbani. Vyakula vya
wachezaji tulikuwa tunapika wenyewe na vyakula vya hotelini tulikuwa tunakula
viongozi, wadau na mashabiki tulioenda nao Misri.
"Wakati tunajiandaa kulala wachezaji wote wakiwa
wameshaingia vyumbani kwao, mie nikiwa chumbani kwangu nikawasha TV nikakuta
zimeongezwa TV stations kadhaa zinaonyesha filamu za ngono. Nilipoona vile
nikajaribu kuanza kupiga simu kwenye kila chumba, nikashangaa kuona simu
inapokelewa mara 1, hivyo nikagundua wachezaji walikuwa macho wanaangalia ule
ujinga, na muda huo ilikuwa saa 7 usiku. Baada ya kugundua hilo jambo
niliwafuata viongozi wenzangu tuliokwenda nao na tukajadili lile suala na kuona
lilikuwa limefanyika kusudi na uongozi wa hoteli ili kuwafanya wachezaji
wasilale mapema na kuwahamasisha kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu,
ukizingatia kwenye ile hoteli juu kabisa na chini kwenye basement kulikuwa na
kumbi za starehe hivyo walikuwepo madada poa.
Aliyekuwa katibu mkuu wa
Simba Kassim Dewji
"Hivyo tulikubaliana na viongozi wenzangu kwamba tuhame hotel ili kuepeukana na mambo yale. Zamalek walipokuja Dar tuliingia contract ya kuwapa hotel waitakayo hapa Dar na wenyewe kutupa hotel tutakayotaka kule Cairo. Hivyo nasi tulipokuwa hatujaridhika na hotel waliyotupa tuliwataarifu na mwanzoni waligoma kubadilisha, lakini kwa sababu mkataba ulikuwa unawabana, ikabidi wakubali kutubadilishia.
"Hivyo tulikubaliana na viongozi wenzangu kwamba tuhame hotel ili kuepeukana na mambo yale. Zamalek walipokuja Dar tuliingia contract ya kuwapa hotel waitakayo hapa Dar na wenyewe kutupa hotel tutakayotaka kule Cairo. Hivyo nasi tulipokuwa hatujaridhika na hotel waliyotupa tuliwataarifu na mwanzoni waligoma kubadilisha, lakini kwa sababu mkataba ulikuwa unawabana, ikabidi wakubali kutubadilishia.
"Wachezaji wote wakahama pale hoteli na baadhi ya
viongozi, wakaenda kukaa kwenye apartments. Viongozi na mashabiki wengine
walibakia pale hotelini. Uzuri wa kuhamia kule kwenye apartments, ambazo kila
moja ilikuwa na vyumba vitatu - ilikuwa rahisi kuwasimamia wachezaji. Kwenye
apartment walikaa wachezaji wawili na kiongozi mmoja. Vyakula tuliendelea kupika
wenyewe.
KUKATAA OFA YA SHOPPING NA KUPELEKWA KUONA
PYRAMID
"Zamalek walikuwa na kila aina ya mbinu katika
kuhakikisha wanawatoa wachezaji katika kuweka umakini kwenye mchezo. Walikuja na
kutueleza kwamba watupeleke shopping tukawajibu kwamba hatukuwa na fedha za
kufanya shopping, wakatupa ofa ya kumfanyia shopping kila mmoja wetu.
Tukawaambie tungekwenda lakini kwa sasa concentration yetu ilikuwa kwenye
kujiandaa na mechi. Pia walitupa ofa ya kutupeleka kuona Pyramid, tukawapa ahadi
ya kwenda siku kadhaa mbele.
"Siku moja kabla ya mechi wakati
tukitoka mazoezini dereva wa basi akaanza kutupeleka kwenye shopping mall,
tulipostukia tukalamzisha apeleke gari hotelini.
ULINZI NA
USHIRIKIANO
"Moja ya vitu vilivyochangia kwa
asilimia fulani kuweza kuwatoa Zamalek ulikuwa ni ushirikiano wa Simba kama
timu, taasisi, wadau wa soka, na watanzania kwa ujumla. Viongozi wote tulienda,
Friends of Simba almost wote walikuwa kule, watanzania wengine ambao sio
washabiki wa Simba kama akina Dr Ramadhan Dau (Pan African), Godfrey na Joseph
Kusaga nao walijumuika nasi kule Cairo kuhakikisha ushindi unarudi
Tanzania.
"Mdhamini wetu mkuu kupitia kampuni
ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji alikuwa nasi bega kwa bega siku zote
tulizokuwa Cairo.
"Tulikuwa tunagawana zamu za kulinda
kila kitu, wakati wa mazoezi viongozi wengine tulienda na timu, wengine walibaki
kuhakikisha kuna usalama katika vyumba tulivyofikia.
"Waziri wa michezo wakati huo Juma
Kapuya na wazira yake kwa ujumla walitupa ushirikiano wote
tuliohitaji."
SIKU YA MECHI -
UWANJANI
"Siku ya mechi kabla hatujaondoka
hotelini tuliongea na wachezaji kuwapa moyo na kuwaweka sawa kisaikolojia.
Mdhamini wetu Mohamed Dewji alitoa ahadi ya kiasi cha fedha kizuri kwa wachezaji
endapo wangeshinda. Hivyo wachezaji walikuwa na kila aina ya sapoti
waliyohitaji. Watanzania kadhaa nyumbani na kule ugenini walikuwa wakituombea
dua na kheri ya ushindi.
"Tuliwahi kufika uwanjani masaa
matatu kabla ya mchezo kuanza, lakini hatukuingia vyumbani. Viongozi kwa
kushirikiana na wadau wengine tulienda kukagua dressing room, tulipiga deki na
kuhakikisha hakukuwa na mchezo wowote mchafu uliofanyika dhidi
yetu.
"Tuliingia vyumbani wakati wa kwenda
kukaguliwa tu na refa kwa sababu ilikuwa ni sheria, lakini wakati huo tulikuwa
tumeshajiridhisha chumba kilikuwa kisafi. Wakati tunaelekea uwanjani, Crescentus
Magori aliamua kubaki chumbani ili kulinda Zamalek wasije kufanya michezo yao ya
kupuliza madawa ndani ya vyumba ambayo huwachosha wachezaji, Magori alikaa mpaka
tuliporudi mapumziko. Kipindi cha pili ndio tukaenda nae uwanjani kwa sababu
Zamalek wasingeweza kufanya chochote kwa kuwa hatukuwa tunarudi tena uwanjani
baada ya kipindi cha pili."
UBORA WA TIMU
"Hayo yote tuliyoyafanya yalikuwa
asilimia 20 tu, asilimia 80 zilizobaki zilibaki uwanjani kwa wachezaji. Kwa
hakika Simba ilikuwa na timu bora, kocha bora na uongozi bora. Siang'a alikuwa
kocha mshindani ambaye hakupenda kufungwa, kwa ushirikiano wetu sote ndio maana
tukafanikiwa.
"Wachezaji walijituma sana pamoja na
vitendo vya refa lakini hawakukata tamaa walijitahidi na kufanikisha kazi
iliyowapeleka uwanjani.
USHAURI KWA
YANGA
"Yanga wana timu nzuri, wanachopaswa
kujituma na kupanga vizuri. Lazima kuwe na ushirikiano mkubwa ndani ya timu, kwa
wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki kwa kushirikiana na
watanzania wote pasipo kujali itikadi za timu.
"Serikali pia inabidi nayo iwape
ushirikiano mkubwa Yanga. Viongozi waache kutafuta sifa binafsi, umoja ni kitu
muhimu, timu inapofanya vizuri kila mtu atapata sifa yake."
SRC
shaffihdauda
0 comments:
Post a Comment