Mijadala mbalimbali kujadili bajeti za wizara mbalimbali, ambapo wabunge wamekuwa wakipata ufafanuzi na majibu ya masuala mbalimbali waliotaka kufahamu kwa undani kutoka kwa mawaziri wa wizara husika.
Yapo mambo mbalimbali yaliibuka katika mijadala hiyo, lengo likiwa kupata majibu ya serikali kuhusiana na maswali yaliyoelekezwa na wabunge kwa maawziri kuhusiana na sekta wanazozisimamia kwani kupitia wabunge ndivyo na wananchi wanavyoweza kujibiwa maswali yao mbalimbali.
Kama tuanvyoelewa kutokana na hali ya ubinadamu, kumekuwa na masuala ya kutofautiana kati ya wabunge wanaouliza maswali na mawaziri au wasimamizi wakuu wa shughuli za serikali bungeni pale ufafanuzi wa kina unapohitajika.
Kutokana na mazingira hayo kumekuwepo na hali ya kurushiana maneno na vijembe kutolewa ama na wabunge au wale wanaojibu kutoka upande wa serikali, matokeo yake kumekuwa na hali ya baadhi yao wasojua au waiokuwa na nguvu ya kujizuia kujawa jazba na hasira.
Kilichonisukuma kuzungumza haya ni tukio lililotokea katikati ya wiki iliyopita baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kurushiana maneno na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, David Kafulila.
Jambo hasa lilisababisha malumbano yao kuwa makubwa zaidi ni pale Jaji Werema alipomuita Kafulila kuwa ni Tumbili huku Kafulila naye akimuita Werema ni Mwizi.
Chanzo cha maneno hayo ya kuidhi kati yao ni baada ya Werema kutoa ufafanuzi, kuhusu fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania(BOT), ambazo zimelipwa Kampuni ya PAP, inayomiliki mitambo ya kampuni ya umeme ya Independent Power Tanzania Limited(IPTL).
Jaji Werema alitoa ufafanuzi wa suala hilo na kusema kuna watu walileta bungeni vipeperushi, wakidai ni ushahidi kuhusu utoaji wa fedha za akaunti ya Esrow na kuhusisha na rushwa na kumtaja Kafulila kuwa ni mmojawao wanaoeneza madai hayo potofu.
Ndipo Mwanasheria Mkuu huyo alipotumia mfano wa kabila la Wanyankole ambapo alisema kuwa kuna usemi wao unaosema’Tumbili hawezi kuamua kesi ya msituni’.
Kabla hajafafanua Kafulila naye aliibuka na kumtaka Werema atyangaze maslahi kwani ni mtuhumiwa, naye Werema alimjibu, “naomba nisikilize, hata kama mtuhumiwa, nina fursa ya kusikilizwa …nisikilize wewe tumbili.” Kafulila naye bila kuwasahs akipaza sauti alisema, “ Wewe(Werema) ni mwizi tu.”
Kwa kweli ni hali ya kusikitisha na kuudhi kwa jamii kuona viongozi hawa waliopewa dhamana ya kutetea maslahi ya wananchi ndani ya bunge, chombo kikubwa chenye hadhi wanafanya mambo ya fedheha kama hayo.
Naamini wote ni watu wazima ambao wanapaswa kudhibiti jazba na hasira zao wanapokuwa wanawajibika kwa ajili ya wananchi, na hakuna mwenye mamlaka au mwenye wadhifa wowote kumkashifu au kumtolea mwingine manneo ya maudhi kama walivyofanya viongozi hawa wawili.
Kwa upende wangu kwa kweli Jaji Werema kwa umri na hadhi yake hakustahili wala hakupaswa kuruhusu hasira na jazba kumtawala kufikia hatua hadi ya kwenda kutishiana nje ya bunge na Kafulila ambaye naamini kwa muonekano wake ni mdogo kwa Jaji Werema.
Tunaambiwa wakubwa waheshimu wadogo na wadogo waheshimu wakubwa, hivyo basi hata Kafulila alipaswa kuwa mstaarabu na kujishusha kusubiri Werema amalize anayosema, kisha angeomba basi Mwanasheria Mkuu amuombe radhi au afute maneno yake, badala nay eye naye kukisa uvumilivu na kumtuhumu mwizi.
Matukio haya ni aibu na fedheha kwa umma wa Watanzania wanaokaa kusikiliza bunge wakiamini wanawakilishwa vyema ili kero zinazowakabili zitatuliwe, lakini wanapoona mambo ya hovyo kama hayo ni dhahiri bunge linashuka hadhi machoni mwa Watanzania ni aibu kwa kweli.
Kwa mtazamo wangu viongozi wanapaswa kujiheshimu lakini kubwa zaidi kuwa wavumilivu na kuheshimiana, kupunguza jazba na hasira hakuna aliyebora kuliko mwingine, kila mmoja anapaswa kufahamu wajibu wake na kuwajibika kwa ajili ya Watanzania ili mwisho wa siku nchi ipate maendeleo
src
Habari Leo
0 comments:
Post a Comment