Baada ya wimbo wa taifa na kusomwa kwa Quran, rais al Sisi alikula kiapo chake ambapo aliahidi kuheshimu sheria na maslahi ya raia wa misri.
Al Sisi alishinda uchaguzi wa urais mwezi uliopita kwa kura nyingi japo idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50.
Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo, Mohammed Morsi.
Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood.
HABARI: BBC
0 comments:
Post a Comment