
Mashambulizi katika eneo la Mpeketoni kenya
Takriban watu 13 wanahofiwa kuuawa katika mashambulizi mawili katika pwani ya Kenya karibu na mpaka wa Kenya na Somali.
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu tisa wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa katika eneo la Gamba kaunty ya Tanariver ,huku wengine wanne wakifariki katika shambulizi kali la ufyatulianaji wa risasi karibu na kituo cha kibiashara cha Kaunty ya Lamu.
Shambulizi la pili lilitekelezwa karibu na eneo la Mpeketoniambapo zaidi ya watu sitini waliuawa mwezi uliopita.
Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi hilo bila ya kutoa maelezo zaidi.
Mwandishi wa BBC nchini kenya amesema kuwa kuna polisi wengi katika maeneo ya pwani kufuatia shambulizi hilo la mwezi uliopita.(P.T
0 comments:
Post a Comment