
Wahudumu wa afya katika tahadhari ya kukabiliana na
Ebola
Benki ya Dunia imetangaza kutoa msaada wa hadi dola milioni mia
mbili, kutoka mfuko wa dharura wa msaada, ili kuzisaidia mataifa matatu ya
Afrika magharibi kukabiliana na ugonjwa hatari wa ebola.
Pesa hizo zitasaidia Liberia, Sierra Leone na Guinea, ili kuboresha vifaa vya
afya ya umma na kushughulikia matatizo ya uchumi yaliyosababishwa na ugonjwa
huo.Rais wa Bank ya Dunia Jim Yong Kim amesema amehuzunishwa sana kwa jinsi Ebola unavyoendelea kuvuruga mfumo wa afya kwa nchi tatu.
Kwa mwaka huu pekee karibu watu mia nane na tisini wamekufa kutokanana Ebola katika nchi za Afrika Magharibi
0 comments:
Post a Comment