
Huku rais Barack Obama akiungana na takriban viongozi 50 kutoka
nchi za Afrika katika mkutano wa kilele, mwanahabari wetu wa BBC Afrika Alexis
Akwagyiram anatathmini kile ambacho Marekani inanuia kutimiza kufuatia mkutano
huo.
Mkutano huo umekuwa ukisubiriwa na wengi tangu Rais Obama kutoa ahadi ya
kuwepo kwa mkutano huo alipozuru Senegal, Tanzania na Afrika Kusini mwaka
uliopita.Tchenga ana hamu kuona yatakayojiri siku za usoni hivyo basi anatafakari kwa kina akijaribu kupata taswira ya siku zijazo.
"Tulipokuja hapa tuligundua kuwa mtazamo watu walio nao kuhusu Afrika ni kuwa Afrika ni mahali pasipo na mwanga- jangwa ambako watu wanaishi na vita, ndwele, na hali makaazi duni,” Tchenga alisema.

Rais Obama alizindua mpango wa kukuza uongozi miongoni mwa
vijana wa Afrika mwaka jana
“Kupitia fursa hii, tumeweza kutoa hadithi zetu na kuonyesha kuwa Afrika ina sauti.”
Tchenga ni kati ya wanafunzi na wanaharakati 500 wa Afrika, waliohutubiwa na Rais Obama siku chache kabla ya viongozi kadhaa walioalikwa kutoka nchi za Afrika kuhudhuria mkutano wa kilele wa siku tatu utakaofanyika Washington, Marekani. Mada ya mkutano huo ni “Kuwekeza kwa kizazi kijacho.”
Wanafunzi hao na wanaharakati watapata mafunzo zaidi na kuwa magwiji bora katika maeneo wanayojihusisha. Marekani pia imekuwa makini kuangazia maswala ya biashara na uwekezaji.
Rais Obama anaamini kuwa kuwa viongozi wa Afrika wana shauku sawa naye.
Obama pia alizindua mpango wa viongozi wa umri mdogo wa Afrika (YALI- Young African Leaders Initiative) akitoa hotuba katika mkutano wa mipango ya mashirikiano uliofanyika tarehe 28 Julai mwaka huu katika hoteli ya kifahari la Omni Shoreham, Washington.

“Usalama na maendeleo na haki tunaotafuta ulimwenguni hayawezi kutimizwa iwapo Afrika haitajitegemea na kujikuza,” Obama alisema akihutubia wanaharakati kutoka Afrika huko Washington.
Kumekuwepo na taarifa kuwa nchi flani hazitohudhuria mkutano huo wa kilele hii leo baada ya kushinikizwa na Rais Mugabe wa Zimbabwe ambaye ni naibu wa mwenyekiti wa Jamii ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Southern African Development Community (Sadc). Pia Mugabe ni naibu wa rais wa Umoja wa Afrika (AU.)
Waziri wa habari wa Zimbabwe Jonathan Moyo alipuuzilia kutoalikwa na Marekani kuhudhuria mkutano huo wa Viongozi wa Afrika kuwa “si jambo,” lakini kutoalikwa huko kumekera baadhi ya watu.
“Tunaelewa kuwa Marekani inalenga kutimiza matakwa yake, na inahofia kuwa Uchina imekuwa kwa haraka na kuongoza katika uhusiano na Afrika,” Mugabe aliarifu Gazeti linalomilikiwa na taifa, Herald.

Mpango huo umeshuhudia vijana zaidi ya 500 wakijiimraisha
katika sekta ya uongozi
Takrimu za hivi punde zinaonyesha kuwa biashara ya Uchina na Afrika ni bilioni $200 ikilinganishwa na $85 Marekani.
Licha ya kuwa na uchumi mkubwa Zaidi ulimwenguni, Marekani ni namba tatu katika orodha kulingana na kiasi cha biashara inaofanya na nchi za Afrika. Uchina na umoja wa Ulaya zinaongoza mbele ya Marekani.
Mhariri mmoja alisema katika Makala ya Gazeti la biashara la Afrika Kusini kuwa huenda Marekani ikakosa “Basi la Afrika” kupitia vitendo vyake.
0 comments:
Post a Comment