MSHINDI wa Big Brother Hotshots, Mtanzania Idris Sultan, hivi sasa anafikiria zaidi maisha yake ya baadaye badala ya kufikiria fedha alizopata katika shindano hilo lililomalizika hivi karibuni Afrika Kusini.
Alisisitiza kuwa ataendelea kuwasaidia vijana walio katika changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga vita madawa ya kulevya, mimba za utotoni na mengineyo.Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili jana kutoka Afrika ya Kusini na kulakiwa na Watanzania katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na maofisa wa kampuni ya Multchoice Tanzania.
Akizungumza pia katika hafla hiyo, Meneja Uhusiano wa Multchoice, Barbara Kambogi, amesema Idris atakuwa chini ya kampuni hiyo kwa miezi kadhaa na kufanya naye kazi katika miradi mbalimbali.
Idris alitoa shukrani nyingi kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla kwa kumpigia kura iliyomwezesha kushinda kitita Dola 300,000 za Marekani.Kujua mengi tembelea www.globaltvtz.com
Idris alitoa shukrani nyingi kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla kwa kumpigia kura iliyomwezesha kushinda kitita Dola 300,000 za Marekani.Kujua mengi tembelea www.globaltvtz.com
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)
0 comments:
Post a Comment