article-2619620-1D8AC3D100000578-532_634x520

Wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla msimu wa Bundesliga haujaisha, weekend hii Borrusia Dortmund ilikuwa ikicheza mechi yake ya mwisho kwenye uwanja wao wa nyumbani Signal Iduna Park dhidi ya Hoffenheim – pamoja na ushindi waliopata siku hiyo, tukio kubwa lilovutia watu ilikuwa sherehe ya kumuaga mshambuliaji wao kipenzi Robert Lewandoski ambaye ataihama timu hiyo mwishoni mwa msimu.
Lewandoski ambaye ni raia wa Poland amemaliza mkataba wake na Dortmund na atajiunga na klabu ya Bayern Munich msimu ujao. Tofauti na wachezaji wengine waliondoka Dortmund ambao walichukiwa na mashabiki – Lewandoski aliagwa vizuri na mashabiki zaidi ya 80,000 waliojazana kwenye uwanja wa Signal Iguna Park na kumfanya kushindwa kujizuia kutokwa na machozi.
Tazama video namna alivyoagwa Lewandoski


src
AyoTZ

0 comments:

Post a Comment

 
Top