
Wanajeshi wa Iraq wakielekea mjini Tiqrit
Serikali ya Iraq inasema kuwa vikosi vyake vimeuteka mji wa
kazkazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa ki-sunni ambao walikuwa wameteka
mji huo wiki mbili zilizopita.
Vyombo vya habari vya kitaifa vimesema kuwa wanajeshi wakisaidiwa na mizinga pamoja na ndege za kijeshi waliwafurusha wanamgambo wa kundi la ISIS na kuwaua zaidi ya sitini.
Waasi hao wamesema kuwa kulikuwa na mapigano makali katika mji huo na kwamba mashambulizi hayo hayakufua dafu.
Iwapo itathibitishwa ,utekaji wa mji wa Tikrit utakuwa hatua kubwa ya jeshi la Iraq tangu ISIS kuyateka maeneo mengi ya Iraq kazkazini mapema mwezi huu.
Serikali sasa inasema kuwa inajiandaa kuelekea mjini Mosul ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo
src
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment