KARIBU miaka 10 iliyopita tuliandika juu ya hatari ya watoto wa mitaani. Kwamba bila mpango wa wazi wa kuwashughulikia watoto hawa, watazalisha familia za mitaani na matokeo yake ni bomu la hatari.
Wakati ule tuliongelea Tanzania ya kesho kana kwamba kesho iko mbali. Sasa tumeanza kushuhudia watoto wa Mbwa-Mwitu na Panya Road.
Wanakamatwa, wanapigwa na kuchomwa moto. Je, hilo ndilo jibu? Tunatafakari zaidi juu ya watoto hawa na maisha yao ya baadaye? Je, tunajali na kuiangalia Tanzania ya kesho ambayo tunataka tusitake ni yetu sote pamoja na watoto wa Mbwa-Mwitu?
Novemba 18, 2004, nikiwa kwenye daladala Jijini Mwanza, nilikwapuliwa pochi yangu, iliyokuwa na pesa si zangu tu bali na za michango ya harusi ya jamaa yangu aliyetarajia kufunga pingu za maisha!
Si lengo la makala hii kuelezea nilivyokwapuliwa pochi hiyo. Ni imani yangu kwamba tukio hili ni la kawaida na limewakumba watu wengine wengi. Wengine wanakwapuliwa simu za mikononi, saa, mikufu ya dhahabu, mikoba yenye pesa n.k.
Tukio la kukwapuliwa pochi hiyo ni tofauti kidogo na lile lililonipata 2002, la kutapikiwa na vijana wa Mererani, kwenye daladala ya Arusha-Moshi. Baada ya tukio hili, nilipofika mwisho wa safari yangu, nguo zilifuliwa na mimi mwenyewe nilioga na kurudi katika hali ya kawaida.
Kukwapuliwa pochi yenye pesa za kukutunza mwezi mzima na nyingine ikiwa ni michango ya harusi halikuwa tukio dogo.
Nimesukumwa kujadili tukio hili na mambo mawili yanayohusiana kwa namna fulani. La kwanza ni kwamba nilimtambua kibaka aliyenikwapulia pochi yangu. Ni mtu niliyekaa naye kiti kimoja kwenye daladala. Niliogopa kumtaja, maana ningefanya hivyo, angepoteza maisha yake palepale. Dadaladala ilikuwa imejaa, na watu hawataki kusikia kitu “mwizi”.
Ninaungama wazi kwamba hata marafiki zangu wa Mwanza, sikuwaambia juu ya ukweli huu kwamba nilimtambua kibaka. Wangeniona mtu wa ajabu kumtambua kibaka na kuamua kukaa kimya. Ukweli huu sasa watausoma kwenye gazeti hili baada ya miaka mingi kupita!
La kujadili hapa ni, je, nilifanya kitendo cha upumbavu kumwachia kibaka kuondoka na pesa ambazo karibu zote hazikuwa za kwangu? Je, ulikuwa ujinga mimi baadaye kushinda ninahangaika huko na kule jijini Mwanza, nikitafuta mkopo wa kulipa pesa zilizokwapuliwa na yule kibaka?
Je, kibaka huyu ni aina ile ya vijana wa Mererani? Je, alizihitaji pesa zaidi yangu mimi? Je, alizihitaji pesa hizo kwa ajili gani? Kunywa pombe na baadaye kuwatapikia watu kwenye daladala?
Je, alizihitaji kuwatunza wadogo zake? Kununua chakula, dawa, kutoa sadaka na zaka kanisani au msikitini? Kulipia kodi ya nyumba? Je, kibaka huyu ni aina ya akina Neema Lukelo, mtoto yatima aliyetoa mada ya kugusa na kuchoma kwenye mkutano wa mwaka (2004) wa Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma (PPF)?
Neema Lukelo, alisema “ Mimi ni mtoto yatima, wazazi wangu wawili wamekufa kwa ugonjwa wa UKIMWI....... kuanzia hapo athari za UKIMWI ziliendelea kunipata bila kujua, mawazo ya mzigo wa kujilea na kulea wadogo zangu yalinijia nikaanza kupoteza mwanga wa matumaini.... nafikiria nitafanyaje juu ya maisha yangu na ya wadogo wangu, nimemaliza darasa la saba nasubiri matokeo na hata kama nikifaulu ni nani atanipa mahitaji muhimu ya shule mimi na wadogo zangu! Ni kweli ndugu wa mama au baba watanipa? Je, walipanga tangu awali? Ni ghafla mno kwao....”.
Je, mtu kama Neema Lukelo, akiamua kuwa kibaka kwa lengo la kupata pesa za kujilea yeye na wadogo zake, akikamatwa, anastahili hukumu ya kifo bila kupata nafasi ya kujieleza na kujitetea? Je, akiamua kuomba ni wangapi watamwamini na kumsaidia?
Yule kibaka aliyekwapua pochi yangu, angenielezea juu ya maisha yake, kwamba yeye ni mtoto yatima na ana jukumu la kujilea yeye mwenyewe na kuwalea wadogo zake, na kwamba hajala mlo wowote kwa siku mbili, hajalipa kodi ya nyumba na mwenye nyumba anatishia kumtupa nje yeye na wadogo zake. Ningeweza kumsaidia?
Je, kama ni wewe umekaa kwenye daladala ungeamini stori ya huyo kibaka na kumsaidia?
Neema Lukelo, aliwauliza swali gumu wajumbe wa mkutano huo wa PPF: “Je, ninyi wazazi wangu ambao mpo hapa ni wangapi kati yenu mnawatunza watoto yatima? Je, matunzo hayo mnayowapa hasa kuhusu elimu ni sawa na mnayowapa watoto wenu? Najua ni vigumu bajeti zenu hairuhusu maana hamkuwa mmepanga hayo, najua hizo ndizo athari za UKIMWI.”
Watoto yatima wanaofanana na Neema Lukelo, ni wengi na wataendelea kuwa wengi. Tunataka tusitake kati yao ndio hao watoto wa Mbwa-Mwitu na Panya Road.
Ni vigumu kuwatambua kwa kuwaangalia machoni. Ni vigumu pia kuwahukumu kwa matendo yao. Mtoto yatima anaweza kuwa na tabia nzuri na mtoto mwenye wazazi akawa na tabia mbaya.
Bila kujenga jamii inayosikiliza, kujali na kujadiliana kuna hatari ya kuyang’oa magugu na ngano nzuri ambayo kama ingeruhusiwa kukua sambamba na magugu ingeweza kuzaa matunda mengi.
Si kila kibaka anakuwa na nia mbaya na si kila kibaka anastahili hukumu ya kifo. Hata hivyo, uhai ni kitu cha thamani kubwa kuliko kitu kingine hapa duniani.
Idadi ya vibaka inaongezeka kadri idadi ya watoto yatima na watoto wa mitaani inavyoongezeka. Matukio ya Panya Road ni kutukumbusha kwamba wapo na ni lazima tuwe na mpango endelevu juu yao.
Ni nani anajali maisha ya watoto yatima? Ni nani anashughulikia maisha bora ya watoto wa mitaani? Tunawaona wakilala na kuishi mitaani, sisi tunapita na kuendelea na shughuli zetu. Watoto hawa wanatoka wapi?
Inawezekana ni watoto wa ndugu zetu, rafiki zetu au watoto wetu. Mitaa, haina uwezo wa kuzaa watoto. Inawezekana kila Mtanzania anahusika kwa njia moja ama nyingine kwa ongezeko la watoto wa mitaani. Watoto hawa, hawana kipato, hawana elimu, hawana chakula, hawana mahali pa kulala. Na mbaya zaidi hakuna wa kuwasikiliza.
Je, watoto hawa wakilazimishwa na hali na kuamua kuwa vibaka tuwakamate na kuwachoma moto? Wakijigeuza kuwa watoto wa Mbwa Mwitu, tuwatafutie askari kuwashika na kuwafunga?
Jambo la pili lililonisukuma kujadili tukio hilo la kukwapuliwa pochi yangu ni kuwashirikisha wasomaji maoni ya rafiki zangu wawili juu ya tukio hili.
Rafiki yangu niliyemjulisha tukio hili akiwa mtu wa kwanza alinitumia ujumbe wa maandishi kupitia kwenye simu yake ya kiganjani : “ Padre Karugendo, umepata fundisho. Tangia leo ukome kuwatetea vibaka na majambazi. Umeongelea shetani na kuuona mkia wake. Ujue kwamba dawa ya vibaka ni moja tu nayo ni kuwachoma moto hadi kufa”.
Rafiki yangu wa pili alikuwa na maoni tofauti kabisa. Huyu alikuwa anafanya kazi kwenye chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross): “ It is true ‘ there is nothing worthy Human life in your pocket’, huwa tunaambiwa sisi Red Cross, tunapokwenda nje kufanya kazi.”
Hoja kuu ni je, tuendelee kuwachoma moto na kuwaua vibaka, majambazi, wezi na wahalifu wengine, tuendelee kuwakamata watoto wa Mbwa-Mwitu na Panya Road na kuwafunga gerezani au watu hawa wapatiwe nafasi ya kutubu, kujirekebisha, kujifunza na kuendelea kutoa mchango wao katika kulijenga Taifa?
Hoja nyingine ya nyongeza inaweza kuwa, je, maana ya utawala bora, utawala wa kisheria ni kuendelea kuwaachia wananchi kuzishughulikia kero zao zote kwa kujichukulia sheria mikononi mwao?
Wakati wa majadiliano ni lazima kuzingatia kwamba matendo ya vibaka, majambazi, wezi na uhalifu mwingine wa aina yoyote ile hayakubaliki katika jamii yetu au jamii yoyote ile iliyostaarabika.
Haya ni matendo yasiyofurahisha, yanavuruga amani na utulivu na kukwamisha maendeleo. Yote haya yakiwekwa kwenye mzani, tunabaki na swali moja la msingi: Tukio la kukwapua pochi, mkufu, saa, simu na mikoba linatosha kuutoa uhai wa mtu?
Ninalopenda kuweka wazi ni kwamba tuna changamoto mbele yetu. Changamoto ya kujenga jamii inayojali, inayojuliana hali, inayochukuliana na kujadiliana. Ni lazima tukwepe kwa nguvu zote kujenga jamii ambayo wachache wanakula na kushiba na kusaza wakati walio wengi wanalala njaa.
Wachache wana nyumba za kifahari wakati walio wengi hawana mahali pa kulala. Wachache wanapata elimu na walio wengi wanabaki bila elimu. Wachache wanaendesha uchumi wa nchi na walio wengi wanabaki kuangalia na kusindikiza.
Jamii kama hii ni lazima izalishe vibaka wengi, majambazi, wezi na wahalifu wa kila aina. Jamii kama hii haiwezi kuwakwepa Watoto wa Mbwa-Mwitu na Panya Road!
Kujenga jamii ni kazi ngumu. Inahitaji watu wa kujitolea, watu wenye upeo, wenye uzalendo watu wa aina ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Watu wasiokuwa na uchu wa madaraka, mali na anasa.
Kujenga jamii ni kazi ya muda mrefu, si kazi ya mtu kufanya na kutarajia matunda ya haraka haraka. Ni kazi ya kila mtu kuchangia kwa kujenga msingi ambao kila jiwe linapangwa kwa vipimo sahihi. Si kazi ya kulipua kama tunavyofikiri na kutenda siku hizi.
Nchi zote zilizofanikiwa kujenga jamii bora zilinufaika kutokana na jasho la vizazi vilivyopita. Ni lazima Watanzania wa leo tukubali kutoa jasho, kupata shida na kujitoa muhanga kwa maandalizi ya Tanzania bora ya siku zijazo. Watoto wa Mbwa-Mwitu na Panya Road ni changamoto, je, tunajali?

src
Raia mwema
See more at: http://www.raiamwema.co.tz/watoto-wa-mbwa-mwitu-panya-road-tunajali#sthash.j8niJ5QO.dpuf
0 comments:
Post a Comment