Moja ya wanavyolalamikia ni suala la wafanyabiashara hao na mamalishe kunyang’anywa vitu vyao katika Operesheni Safisha Jiji, iliyofanyika hivi karibuni.
Suala lingine pia ni la waendesha bodaboda kutoruhusiwa kuingia katikati ya mji, kwa lengo la kuondoa msongamano na kudhibiti vitendo vya kihalifu, vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya waendesha pikipiki hao.
Wakiwa katika mkutano maalumu ulioandaliwa na CCM Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, licha ya kutishia kutowapigia kura, pia walimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, kujiuzulu wadhifa wake huo.
Ni dhahiri kuwa katika operesheni hiyo ya kusafisha jiji, kuna masuala mengi yalifanyika, ikiwemo kuwanyang’anya mali wafanyabiashara na kukimbia nazo, bila kuwapatia na kulipia faini kidogo.
Lengo la kuwaondoa mamalishe na wafanyabiashara hao ni kuhakikisha kila biashara inafanywa katika maeneo yaliyoruhusiwa kwa manufaa ya jiji na wananchi wake.
Tunakubaliana wote kuwa ni lazima kuwa na sheria na taratibu katika kuongoza watu, hivyo kuna sehemu zimeruhusiwa kufanya biashara na zingine hazijaruhusiwa.
Hivyo, kuacha kila mtu kufanya biashara anapopenda ni dhahiri itakuwa uchafu na watendaji wa jiji kuonekana hawafanyi kazi.
Kuhakikisha wanasimamia kazi walizopewa, Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji lazima watimize wajibu wao kwa kusimamia Sheria na kukabiliana na wote wanaovunja Sheria, kwa kuwaondoa maeneo yasiyoruhusiwa.
Hivyo suala la kutishia serikali iliyopo madarakani kwa kuwanyima kura ni kumaanisha kuwa serikali iwaache watu wavunje sheria, bila kuwasimamia kwa hofu ya kunyimwa kura mwakani.
Ni vema kila mmoja akafikiria kuwa watendaji wangeacha kusimamia sheria kwa hofu ya kunyimwa kura, nchi ingekuwa katika hali gani, kwa kila mtu kufanya anachoweza na serikali kumuangalia tu bila kuchukua Sheria.
Mimi naamini kuwa wafanyabiashara, bodaboda na mamalishe, walikuwa na hoja ya kulalamikia baadhi ya vitendo walivyofanyiwa vya kuchukuliwa mali zao, hivyo kuwafanya washindwe kuendelea na biashara zao.
Malalamiko hayo yalikuwa na mashiko, kwani wameshindwa kwenda katika sehemu zilizoruhusiwa na kuendelea na biashara kwa ajili ya maisha ya kila siku, lakini siyo kulalamikia operesheni na kutaka waachwe wafanye wanachotaka.
Waendesha bodaboda hao, pia kweli wamekosa biashara kwa kutoingia katikati ya miji. Lakini, ni lazima kukubaliana kuwa ili kuendesha jiji na kuhakikisha usalama unakuwepo, ni lazima kuwe na Sheria na taratibu zilizowekwa.
Kutokana na suala hilo, ni vema wananchi tukaangalia kutoingiza masuala ya siasa katika utendaji, kutokana na kuwa usimamiaji wa sheria ni suala la kiutendaji. Hivyo, kutishia kutowapa kura wasimamizi wa sheria ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.
Wakazi wa jiji hili, wote tunapenda kuona likiwa safi na linalopitika kwa urahisi. Lakini, bila watendaji kusimamia sheria, hatuwezi kufikia malengo hayo.
Nawasihi pia wanasiasa kuwa makini, hasa kipindi hiki nchi inapoelekea katika uchaguzi mkuu ujao, kwa kutokubali kuyumbishwa na kuwafanya watendaji washindwe kutimiza wajibu wao, kwa ajili ya kutaka kura mwakani.
Nasema hivyo, kutokana na kauli ya Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Busaro Pazi ya kuwataka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Jiji, kujiuzulu kwa kutowatetea wanyonge, suala ambalo si kweli kwani watendjai hao wanasimamia Sheria.
Jambo la msingi ni kuwatafutia ufumbuzi wa kweli wapigakura, kwa kufanya biashara maeneo yaliyoruhusiwa
src
Habari
0 comments:
Post a Comment