Wakati Watanzania wanalala na kubaki kulalama kuwa maisha magumu, huku wakiwaza namna ya kufika peponi bila kufa,
wenzetu huko wanakesha wakitafakari wavumbue nini kitakacholeta maendeleo ya haraka.
Tumeshuhudia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakisema wanakusudia kuweka maroboti kuongoza magari, lakini wenzetu huko Ulaya wamekuja na ubunifu mpya wa kisayansi ambapo sasa wanataka kuingiza barabarani magari yasiyotumia dereva na yasiyotumia betri za kawaida, bali umeme.
Unashangaa? Magari hayo yanatumia teknolojia inayoitwa "flow-cell" ambapo yatakuwa na matenki mawili yenye vimiminika tofauti vinavyohifadhi nguvu ya umeme. Vimiminika hivyo vinapita katika ufito mwembamba baina ya matenki hayo mawili, na kutengeneza chaji ya umeme.
Magari hayo hayatatoa moshi wa aina yoyote na hivyo kuonekana bora katika kutunza mazingira, kasi yake ni meta 217 kwa saa na mfano upo kwa gari inayofanana na Nissan GT-R Nismo. Kampuni ya Nanoflowcell, iliyoko Ujerumani, inasema teknolojia hiyo ina uwezo wa kutoa umeme mara tano ya betri za kawaida, na haina madhara. Gari inaweza kusafiri kwa mile 372 kwa kuchajiwa mara moja tu na tayari yamethibitishwa kwenye barabara za Ulaya.
Lakini ukiachana na hilo, tayari kuna magari ambayo yametengenezwa na hayajaingizwa barabarani ambayo yatakuwa hayatumii madereva.
Tayari Uingereza imesema itayaruhusu magari hayo kuanzia Januari mwakani kwa majaribio kuona kama inawezekana. Watu mtakuwa mkipanda halafu gari linajitekenya lenyewe na kuchapa mwendo, imekaa sawa hiyo, au vipi!

Jeshi la Marekani na Marine Corps limefanya majaribio ya mfumo unaojulikana kama Autonomous Mobility Appliqué System (AMAS) kwenye makao makuu ya kampuni ya Ford Hood, Texas.
Kitengo cha Utafiti wa Magari ya Jeshi, Maendeleo na Uhandisi cha nchi hiyo kinataka kuibuka na magari ya kivita ambayo yatakuwa yanajiendesha yenyewe, mpango ambao wanataka ukamilike ifikapo mwaka 2025, na kinatumia teknolojia iliyoanzishwa na Lockheed Martin kuendesha malori yenye uwezo wa kubeba makombora ya kijeshi.
Tanzania tutawezea wapi kuwa na magari yanayojiendesha ukizingatia mifoleni iliyojazana hivi! Labda magari yasiyotumia betri yanaweza kutufaa kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mikweche iliyojaa tele nchini, tena wengi wakiwa wanaimiliki kwa mikopo ya SACCOS!
(MNYAMA)

0 comments:
Post a Comment